MTANGAZAJI

MAKAMU WA RAIS AWATAKA WANAWAKE NCHINI TANZANIA KUPIMA AFYA ZAO

 

Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati
wa kuhitimisha mashindano hayo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan
akishiriki mbio za NBC Dodoma Marathon

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan
(katikati)akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Julius
Mwaisalege (wakwanza kushoto) mfano wa hundi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya
mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake nchini humo  kujitokeza kupima afya zao mapema ili kujua hali zao hatua inayosaidia kupambana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi. 

Mama Samia ametoa agizo hilo wakati akiwahutubia wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dodoma Marathon zilzofanyika Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma.


“Akinamama mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu wetu” amesema Mama Samia.


Katika mashindano hayo, Makamu wa Rais Mama Samia amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo hatua inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi nchini.

Makamu wa Rais Mama Samia amesema mashindano ya NBC Dodoma
Marathon yamekuja muda mwafaka hatua inayosaidia wanamichezo kujiandaa vema katika mashindano ya Olimpik yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni 2021 Tokyo nchini Japan pamoja na kuchangisha kiasi cha takriban zaidi ya Sh. milioni 75 ambazo zimeelekezwa kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar es salaam kusaidia mapano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.


Naye Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalege amemhakikishia Makamu wa Rais Mama Samia kuwa fedha zilizopatikana kutokana na usajili wa wanariadha wa mbio za NBC Dodoma Marathon zitatumiwa na kufanyiwa kazi iliyokusudiwa ili kuokoa maisha ya wanawake nchini.

Dkt. Mwaisalege amesema fedha hizo zinalenga kutoa elimu ya ugonjwa wa saratani, kufungua vituo 25 na kuandaa wataalamu 100 watakaosaidia wananchi kupima saratani ya mara kwa mara hatua itakayosaidia kuepukana na ugonjwa huo na wakigundulliwa kuwa nao waweze kutibiwa mapema na kupona ili waendelee na shughuli zao za kimaendeleo.


Mbio hizo za NBC Marathon zimehusisha wanariadha 3000 wakijumuisha wanariadha kutoka Tanzania kati yao  19 kutoka nchini Kenya, 12 kutoka Uganda pamoja na wanariadha wanne kutoka Malawi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.