MTANGAZAJI

ZIARA YA AMBASSADORS OF CHRIST NCHINI MAREKANI MWEZI AGOSTI 2018Waimbaji wa  Ambassadors of Christ toka Kigali,Rwanda wanatarajia kuwasili mjini Dallas hapa Marekani alhamisi ya jumahili Agosti 2 mwaka huu, kwa ajili ya mkutano wa Injili utakofanyika mjini Dallas na Huston jimboni Texas.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kwaya hiyo inayopendwa na hasa na watu wanaotoka Afrika Mashariki na Kati wanafahamu Kiswahili,Kinyarwanda na Kifaransa toka kuanzishwa kwake mwaka 1995 huko Rwanda.

Naye Mhutubu wa mikutano hiyo toka Dar es salaam,Tanzania Dr Herry Muhando amekwisha wasili kwa ajili ya  mikutano hiyo ambayo itafanyika kuanzia Agosti 5 mwaka huu ikiandaliwa na Waadventista Wa Sabato toka nchi za Afrika Mashariki na Kati walioko Dallas na Huston.


Mbali na kuimba katika mikutano hiyo ya Injili  waimbaji wa Ambassadors of Christ watashiriki kuimba katika matamasha matatu hapa Marekani.

Ziara ya waimbaji hawa inakuja siku chache tu baada ya mwimbaji mahili wa sauti ya kwanza wa kwaya hii toka Kanisa la Waadventista Wa Sabato Sarah Uwera ambaye huimba na kaka zake wawili kufunga ndoa huko Rwanda hivi karibuni.


-->

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.