GGM NA TACAIDS KUZINDUA KILIMANJARO CHALLENGE 2018
![]() |
Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo. |
![]() |
Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakijadili jambo mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema leo. |
![]() | ||||||||
|
Akizungumzia tukio hilo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alisema shughuli hiyo itafanyika Mei 4, 2018 katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam. Dk. Maboko alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka 2017 baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro. .
Aliongeza kuwa, ili kushiriki Kili Challenge, muhusika anaweza kuchangia mfuko huu kwa kujifadhili au kumfadhili mwingine kupanda au kuendesha baskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro. Kuwa sehemu ya mafanikio.
Kwa mawasiliano zaidi au kutoa mchango wasiliana nasi kupitia email: GGMkilichallenge@anglogoldashant.com, au tovuti www.geitakilichallenge.com. Geita Gold Mine na TACAIDS tunatumia mwamvuli huu wa Kilimanjaro Challenge katika kuelimisha jamii kuhusu janga hili la VVU/Ukimwi na tunatarajia siku moja Tanzania itatangaza kuisha kwa maambukizi ya VVU/ UKIMWI. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.geitakilichallenge.com
Post a Comment