DAR ES SALAAM:MARAZA JIPYA LA MAWAZIRI TANZANIA LAWAACHA MAWAZIRI WANNE
Rais Magufuli ametangaza baraza
jipya la mawaziri huku kukiwa na mabadiliko kidogo ambapo amewaondoa
mawaziri wanne waliokuwa kwenye baraza la awali.
Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye hayupo kwenye baraza hilo la Mawaziri na nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga
Lilifuatalo
ni Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.
1. Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
I.
Waziri – George Huruma Mkuchika
2. Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
II.
Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
III.
Naibu Wazri - George Joseph Kakunda
3. Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
I.
Waziri - January Yusuf Makamba
II.
Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola
4.
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Walemavu.
I.
Waziri - Jenista Joackim Mhagama
II.
Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
III.
Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
5. Wizara ya
Kilimo.
I.
Waziri - Dkt. Charles John Tizeba
II.
Naibu Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa
6. Wizara ya
Mifugo na Uvuvi.
I.
Waziri - Luhaga Joelson Mpina
II.
Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
7. Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
I.
Waziri - Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
II.
Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
III.
Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa
8. Wizara ya
Fedha na Mipango.
I.
Waziri - Dkt. Philip Isdor Mpango
II.
Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji
9. Wizara ya
Nishati.
I.
Waziri - Dkt. Medard Matogoro Kalemani
II.
Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu
10.
Wizara ya Madini.
I.
Waziri - Angellah Kairuki
II.
Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo
11. Wizara ya
Katiba na Sheria.
I.
Waziri
- Prof. Palamagamba John
Aidan Mwaluko
Kabudi.
Kabudi.
12.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
I.
Waziri - Dkt. Augustine Philip Mahiga
II.
Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba
13.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
I.
Waziri - Dkt. Hussein Ali Mwinyi
14.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
I.
Waziri - Mwigulu Lameck Nchemba
II.
Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
15.
Wizara ya Maliasili na Utalii.
I.
Waziri - Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
II.
Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga
16.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
I.
Waziri - William Vangimembe Lukuvi
II.
Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula
17.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
I.
Waziri - Charles Paul Mwijage
II.
Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya
18.
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
I.
Waziri - Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
II.
Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha
19.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto.
I.
Waziri - Ummy Ally Mwalimu
II.
Naibu Waziri - Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile
20.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
I.
Waziri - Dkt. Harrison George Mwakyembe
II.
Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza
21.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
I.
Waziri - Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
II.
Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla
ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw.
Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa
kazi nyingine.
Wateule wote
wataapisha Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment