KAMPALA:MWIMBAJI WA THE LIVING VOICES AZIKWA KIJIJINI KWAO
Waimbaji wa The Living Voices wakiwa na Mwimbaji toka Tanzania Fadhili huko Kayunga kwenye shughuri ya Mazishi ya Nyombi Steven |
Mamia ya
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato na Madhehebu mengine Oktoba 7 mwaka huu wameshiriki katika maziko ya Mwimbaji
Mahiri wa Sauti ya Tatu wa kwaya ya nyimbo za Injili The Living Voices ya
nchini Uganda Nyombi Steven aliyefariki
juzi usiku baada ya kugongwa na gari wakati akielekea nyumbani baada ya kutoka
Kazini.
Nyombi amezikwa kijiji kijijini kwao Kayunga umbali wa mile 45 toka jiji la Kampala Uganda huku tukio hilo likishuhudia zaidi ya kwaya 10 za madhehebu tofauti tofauti zilizoimba usiku kucha
Marehemu
Nyombi aliyezaliwa miaka 45 iliyopita alianza kuimba na Kwaya ya Jerusalem Pipers na
alikuwa ni Miongoni mwa waimbaji waanzilishi wa The Living Voices ambayo nyimbo
zao husikika kupitia Morning Star Radio na Morning Star TV alililelewa Shangazi
yake ambaye ni mwimbaji na analala mauti akiwa amedumu katika kwaya hiyo kwa
muda wa miaka 16 na ameacha mjane na watoto sita,wakike wanne na wakiume wa
wawili.
Post a Comment