MTANGAZAJI

VIDEO YA MPYA YA KWAYA YA VIJANA NYARUGUSU TANZANIA HII HAPA

Juni 16 mwaka huu,kwa mara ya kwanza JCB Studioz kupitia channel yao ya Youtube wamesambaza video mpya ya wimbo wa Mji Mtakatifu ulioibwa na Kwaya ya Vijana ya Nyarugusu,Geita nchini Tanzania.

Santuri mwonekano ya kwaya hiyo iitakayoitwa Amri Kumi inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa nyimbo za Injili baada ya kwaya hiyo kuimba kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Ushindi Hatimaye uliokuwa ukirushwa mubashara na Morning Star Radio na Morning Star Tv tokea Mabatini jijini Mwanza ambapo kwaya zaidi ya 120 zilihudumu.

Toleo hilo lenye nyimbo tisa ambazo video yake ilifanyika katika maeneo mbalimbali huko Nyarugusu ,Geita pamoja na Geita Mjini ikionesha baadhi ya sehemu za Ziwa Victoria ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa duniani.

Akizungumza akiwa jijini Nairobi nchini Kenya  hii leo Moses Romeo ambaye ndiye mwongozaji na mtayarishaji wa video hiyo amesema kwa sasa yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha santuri hiyo mwonekano.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.