MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:KUPANDA MABASI YA MWENDO WA HARAKA JIJINI SASA NI KWA KADI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart),  David Mgwasa (kushoto),akionesha kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo uliotarajiwa kuanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART,  David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart  katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

"Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu

Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.

Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.