KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI YUKO NCHINI RWANDA
Kiongozi wa Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Duniani Mch Ted Wilson ameweka jiwe la Msingi la Chuo Kipya cha Udaktari cha Waadventista nchini
Rwanda
Wilson ambaye ni mara yake
ya pili kufika nchini humo toka awe Kiongozi wa Kanisa hilo baada ya kufanya
hivyo mwaka jana aliweka jiwe hilo la msingi kwenye jengo la Chuo hicho ambalo
litagharimu dola za kimarekani milioni 6.1 liko Masoro kwenye Chuo Kikuu cha
Waadventista Wa Sabato cha Afrika Mashariki na Kati cha Kigali,Rwanda .
Sehemu ya kwanza ya ujenzi
wa chuo hicho itahusisha sehemu ya wanafunzi wa kike na wa kiume,eneo la kulia
chakula,mahali pa kulala wageni,na
litafunguliwa kwa ajili ya wanafunzi Septemba 2017.
Kiongozi huyo ambaye
ameambatana na mkewe Nancy amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Rais wa
Rwanda Paul Kagame atakuwa nchini
humo ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake katika mikutano ya injili ya majuma
mawili iliyoanza ijumaa jioni
ambapo watu 100,000 wanatarajiwa kubatizwa ifikapo Mei 28 mwaka huu.
Post a Comment