MTANGAZAJI

MWILI WA MTANZANIA ALIYEPIGWA RISASI NCHINI MAREKANI WAAGWA NA KUSAFIRISHWA KUJA TANZANIA

Jioni ya Jumamosi (16/04/2016) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada katika Kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. 

Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry ulitarajiwa  kusafirishwa jioni ya Aprili 17,2016 kwa saa za Marekani kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa Tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.

Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani

Wachungaji wakiwa nje ya kanisa kabla ya ibada

Jeneza lililobeba mwili wa Henry likiingizwa kanisani
Dada  Lulu  ( mdogo wa Marehemu Henry ) akimuaga kwa uchungu kaka yake
Mr. & Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani
Waombolezaji wakilia kwa uchungu
Rafiki wa Henry kutoka Cameroon
Waombolezaji


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.