MTANGAZAJI

HISTORIA YA SURUALI ZA JEANS NA VISHIKIZO KWENYE MIFUKO YAKE HII HAPA

 

Mavazi aina ya Jeans haswa Suruali zilitengenezwa nchini Marekani kwa mara ya kwanza kwa ajili ya wafanyakazi wa kipato cha chini kwa sababu zilikua ngumu , zinazodumu na zinazoweza kuhimili mengi .

Hata hivyo kwa kipindi hicho ilikua ni kawaida kwa mifuko ya suruali kuchanika kutokana na shuguli au vitu , ilikuwa ni tatizo kwa sababu mifuko ilitakiwa .

Kutokana na hilo fundi wa nguo bwana Jacob Davis , aliyekuwa mteja wa Levi Strauss & Co.( watengenezaji wa Jeans ) alikuja na wazo la kumaliza tatizo la kuchanika mwaka 1873 .

Yeye alitengeneza vishikizo vya shaba kwa pembeni ili mifuko isiwe inachanika wala kudondoka kiurahisi .

Jacob alitaka kuwa na hati miliki na ugunduzi huu lakini hakuna na uwezo wa fedha , kwahiyo mwaka 1872 aliwaandikia barua Levi Strauss kuwaeleza ili wamsaidie kulipa wafanye biashara .

Levi Strauss Walikubali na kuanzia siku hiyo suruali zilikua na vishikizo vya shaba kwa pembeni .

Na Yona Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.