MAHOJIANO NA DC PAUL MAKONDA KATIKA KIPINDI CHA JUKWAA LANGU DEC 7,2015
Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki, tumeungana na Mhe Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jiji Dar Es Salaam ambaye mbali na mambo mengine, ameeleza "ya moyoni" kuhusu tofauti iliyopo kati ya utendaji wa Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Kikwete (aliyemteua katika wadhifa huo) na Rais wa sasa Dk John Magufuli. Kabla ya hapo aligusia namna alivyoteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya, na kwanini anaamini inastahili kuwepo namna nzuri zaidi ya kuteua watu katika nafasi kama yake.
Na kabla ya hayo yote, alizungumzia migogoro mbalimbali inayoendelea wilayani mwake kama wa kiwanda cha Urafiki, kubomolewa kwa nyumba za thamani, mgogoro wa Coco Beach nk.
Na kama ilivyo desturi, akapokea maswali na ushauri toka kwa wasikilizaji wetu
KARIBU
Post a Comment