MTANGAZAJI

WADAU WA MUZIKI WA INJILI KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WASHTUSHWA NA KIFO CHA MWALIMU EPAINENTO MUJAYA

Wadau wa Muziki wa Injili katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki wamepata pigo jingine juma hili la kuondokewa na  Mtunzi wa Nyimbo,Mwalimu,Kiongozi wa Kwaya na Kiongozi Mkuu katika chama cha Vijana wa Kanisa hilo atakayekumbukwa daima Epaineto Mujaya ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiifundisha Kwaya ya Kamunyonge ya mjini Musoma.

Epaineto Mujaya (Pichani)ambaye anatoka katika familia ya waimbaji akiwemo kaka yake Balthimayo Mujaya aliyewahi kuwa Mwalimu wa Kwaya ya Kamunyonge,Mshahidi na Kirumba ambaye pia ni Marehemu.

Marehemu Epaineto alifariki usiku wa kuamkia jana Oktoba 8,2015 huko Musoma,Mara Tanzania.Marehemu aliyejiunga na Kwaya ya Kamunyonge mwaka 1985 huku akiwa pia amewahi kufundisha kwaya ya Mwisenge,Ikizu na Balili akishirikiana na Mwalimu Gerald Joro.

Epaineto anatarajia kuzikwa Oktoba 11 huko Musoma,Mara Tanzania

Mtazamo News . Powered by Blogger.