UGUNDUZI WA MAPEMA WA SARATANI YA MATITI UTAOKOA MAISHA YAKO
Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitali za Apollo
Saratani inasemwa kuwa chanzo kikubwa cha pili kinachosababisha vifo ulimwenguni. Saratani ya matiti peke yake inaripotiwa kuwa ya pili kama sababu kubwa ya vifo vinavyohusisha saratani kwa wanawake nchini
Tanzania. Kuchelewa kupata ugunduzi wa haraka na tiba kwa wagonjwa wengi wa saratani ya matiti kunachangia kuleta ugumu kwenye matibabu
pale ugonjwa unapoingia ngazi ya juu zaidi.
Gonjwa hili limeendelea kuwa janga hasa kwa nchi zinazoendelea.
Ulimwenguni,mwezi Oktoba ni mwezi maalumu wa kutoa maarifa na elimu juu ya saratani ya matiti.
Kwa kawaida tarehe 19 Oktobanikilele cha saratani ya matiti nalengo kuu likiwa ni kutoa maarifa ya msingi na yenye faida kuhusiana na ugonjwa huo.
Silaha bora ya kupigana na saratani ya matiti ni kuigundua mapema.
Ongezeko kubwa la
namba ya vifo kutokana na saratani linatikisa Tanzania,
jinsii navyoathiri namba kubwa ya wanawake kwa sasa.
Kutokana na takwimu za hivi karibuni kutoka hospitali ya Ocean Road kitengo cha saratani
(ORCI), tafiti zinaonyesha ongezeko kubwa la namba kutoka mwaka 2013-2014 (nusu ya kwanza
ya mwaka) zaidi ya kesi mpya 400 zimeripotiwa.
Maoni kwenye hizo takwimu, Dk. Crispin Kahesa mkurugenzi wa Ocean National Health Insurance Fund alisema kutokana na wingi wa vifo vitokanavyo na saratani, lazima kuwe najitihada shirikishi zakupigana na saratani ya matiti.
Kuhamasisha njia bora
za afya kwenye matukio kama haya imekuwa ni wajibu mkuu kwa hospitali za Apollo ambazo zimetunukiwa tuzo za kimataifa.
Katika kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu maada hii, mkurugenzi wa hospitali za Apollo, Suneeta Reddy, amesema kwa miaka sasa,saratani ya matiti imedhihirika kuwa moja ya janga kubwa kwa wanawake wote ulimwenguni. Ni muhimu kwa wanawake wote kujali afya zao maana wanamajukumu makubwa sio tu kwenye familia ila pia kwenye jamii kwa ujumla. Wajibu wa mwanamke mara zote haupo tumuhimu kwenye maisha ya familia ila pia kwenye nyanja za jamii na uchumi hasa kwa nchi zinazoendelea.
Ukosefu wa elimu na hamasa umesababisha wimbi kubwa
la wanawake kukosa fursa ya kugundua mengi kuhusu saratani ya matiti. Njia pekee ya kufanya hayo ni kupata elimu sahihi na uelewa wa
kina kuhusu nini ni saratani ya matiti.
Elimu yakutosha inatakiwa itolewe kwa jamii kusaidia kupunguza zigo la ugonjwa huu. Saratani ya matiti kama isipogundulika mapema itapelekea kifo moja moja. Alisema Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitaliza Apollo.
Elimu yakutosha inatakiwa itolewe kwa jamii kusaidia kupunguza zigo la ugonjwa huu. Saratani ya matiti kama isipogundulika mapema itapelekea kifo moja moja. Alisema Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitaliza Apollo.
Hebu tuanze kufanya kitu sasa hivi.
Chagua njia ya ugunduzi, jifanyie uchunguzi mwenyewe wa saratani ya matiti au kwa kutumia kifaa kijulikanacho kitaalamu kama
mammogram hiki ni chombo madhubuti kitakacho saidia kugundua ugonjwa katika ngazi ya awali kabisa,
alisema mkurugenzi Suneeta
Reddy.
Ugunduzi wa saratani ya matiti mapema kwa kutumia kifaa cha mammography kumepunguza vifo vingi kwa wanawake ambao walionekana hawana dalili zozote waliokuwa na uvimbe na waliokuwa hawana uvimbe kwaile ngazi ya kwanza.
Mkg.SuneetaReddy anawataka watanzania wote tuheshimu na tutenge dakika tano tu za kujifanyia uchunguzi, alisema.
Kwa kushirikiana na wito wa Mkg. Suneeta
Reddy kuhusu ugunduzi wa saratani ya matiti katika ngazi ya awali, mkuu wa idara ya mionzi katika taasisiya
Ocean Road, Dk. Yekebeth Vuhahula,
aliongeza kuwa saratani ya matiti bado ni changamoto kubwa Tanzania
kwasababu wanawake wengi wanashindwa kujitokeza mapema kwa matibabu. Kwa jinsi ambavyo saratani ya matiti inazidi kukomaa na kusambaa,
ndivyo inasababisha nafasi ndogo ya matitabu kufanya kazi. Kama
saratani ya matiti ikigundulika mapema inatibika kirahisi.
Kwa ujuzi wake
kuhusu wagonjwa wa saratani ya matiti Tanzania, wanawake wa Tanzania wanaoufahamu mdogo na wengine hawana ufahamu kabisa kuhusiana na vitu hatarishi,
dalili, na matibabu ya saratani ya matiti. Imani
potofu kutoka kwenye jamii na tamaduni ni sababu nyingine zinazopelekea saratani ya matiti kuwa sugu kwa wanawake hapa nchini.
Kuhusu Hospitaliya Apollo
Hospitaliza Apollo ni za kwanza
katika eneo la Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot,
ambayo ni aina ya upasuaji isiyo kuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot
iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Taasisi inawataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji,
upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora
kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci
inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo
(Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo,
na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.
Post a Comment