DAR ES SALAAM:WANANCHI WA KISARAWE WASHIRIKI MDAHALO WA AJENDA YA WATOTO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015
Ndg
Abel Mudo, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CCM akichangia
katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo ulihusisha pia wakazi wa kata
ya kisarawe
|
| ||
Mwanafunzi
Amina Joka akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo
wanafunzi wa shule za Msingi chanzige A ,chanzige B na kisarawe na
wagombea wa udiwani kupitia vyama vya ccm na chadema walishiriki
Ndg
Abel Mudo ambaye ni mgombea wa Udiwani kupitia CCM akichangia katika
mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wanafunzi wa
CHANZIGE ,na kisarawe
|
Mmoja
wa wanafunzi wa shule msingi Changize A akifuatilia kwa makini mdahalo
wa ajenda ya watoto uliowahusisha wagombea wa udiwani wa vyama vya CHADEMA na CCM
|
Ndg
.Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA
akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na
wanafunzi
|
Picha
za Wanafunzi ni za wanafunzi wa shule za msingi Chanzige A, Chanzige B
na Kibasila zilizopo Kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo huo.
|
Ndg
.Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA
akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na
wanafunzi
|
Ajenda
ya watoto ilianzishwa na mashirika ya watoto Tanzania yakiongozwa na
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa nia ya kuhakikisha
maswala ya watoto na haki zao yanawakilishwa vyema katika serikali ya
Tanzania.
Katika
kuhakikisha kwamba Ajenda za watoto zinazungumzwa katika jamii Kipindi
cha redio cha Walinde Watoto jana kilifanya mdahalo uliowahusisha
wagombea wa udiwani kata ya Kisarawe ambao ni Abel Mudo (CCM) na Baraka
Musa (CHADEMA) na wakazi wa Kata ya Kisarawe ili kujadili changamoto
mbalimbali zinazowakabili watoto na mipango ya vyama vyao katika kutatua
changamoto hizo.
Mdahalo
huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
ulihudhuriwa na wenyekiti wa vijiji, na vitongoji, walimu, maafisa
ustawi wa jamii pamoja na wananchi wakazi wa Kata ya Kisarawe.
Mwanafunzi
Amina Joka aliwataka wagombea udiwani hao pindi mmoja wapo
atakapochaguliwa, wahakikishe wanajenga hosteli za wanafunzi kufikia
kwani kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali mrefu sana kwenda shule hali
ambayo ni hatarishi kwani wanakutana na vishawishi vingi njiani.
Unaweza
kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio
shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi
kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org
Post a Comment