MWANZA:UN NA SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI ILIYOPO NCHINI
Mgeni
 rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira 
Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja
 wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya
 kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kwenye
 maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani  ambapo kitaifa yamefanyika 
jijini humo na kuandaliwa na Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT)
 kwa ushirikiano wa UNESCO ambapo yaliwashirikisha Viongozi wa Serikali,
 Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Viongozi wa madhehebu ya dini, 
Jeshi la Polisi, Walemavu, Wananchi pamoja na  Ofisi ya Msajili wa vyama
 vya siasa. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis 
Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya
 siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia.(Picha zote na Zainul 
Mzige wa Modewjiblog).
Umoja
 wa Mataifa (UN) umesema utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania
 kulinda na kudumisha amani ya pamoja kwa makundi yote ili amani iliyopo
 itumike kuleta maendeleo endelevu nchini.
Hayo
 yamebainishwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la 
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
 Zulmira Rodrigues,  wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya
 siku ya Amani Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza (Septemba 
21.2015).
Bi.Rodgrigues
 amesema amani ya pamoja inatoa nafasi kwa kila mmoja kuwa mshirika wa 
kudumisha na kuendeleza amani bila kujali itikadi, imani au matabaka 
mbalimbali yaliyipo ndani ya jamii.
Amefafanua
 kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kulinda amani, hivyo nguvu ya 
pamoja ni muhimu katika kufikia malengo na maendeleo yanayotakiwa 
kutokana na kuwepo kwa utulivu, mshikamano, umoja, na amani.
Kwa
 upande wake, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi 
amewataka watanzania kuachana na propaganda za kisiasa zinazoleta chuki 
na hasa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Jaji
 Mutungi ameeleza kuwa amani haina tabaka na kusisitiza umuhimu wa 
wananchi kupiga kura kwa kutumia falsafa ya kulipenda taifa na kuwaonya 
viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuwadharau watanzania ambao 
wameilinda amani kwa muda mrefu.
Nalo
 Jeshi la Polisi mkoani humo, limelaani kitendo kilichofanywa na watu 
wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kwa kushambulia polisi 
na kuvunja vioo vya gari la polisi kwa kusingizio cha kampeni za 
uchaguzi.
Katika
 tukio hilo  imeelezwa kuwa,  baada ya watu waliokuwa wakitokea katika 
mkutano wa kampeni wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kushambulia 
Polisi, kuvunja vioo vya gari la polisi na kujeruhi askari.
Mkuu
 wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akisoma hotuba kwa niaba ya 
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye maadhimsho ya siku 
ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Mkuu
 wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
 Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akitoa ujumbe 
maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco, Irina 
Bokova kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani 
Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda
 wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo 
akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani 
Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
 Msajili
 wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake 
kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa 
yamefanyika jijini Mwanza.
Jukwaa
 kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku
 ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akiteta jambo na Mgeni
 rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira 
Rodrigues wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya 
Amani, ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza 'Amani' ikitolewa.
Kaimu
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga akiweka saini kwenye Azimio 
maalum la kuenzi Amani lililoandaliwa kwenye maadhimisho hayo huku Mgeni
 rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira 
Rodrigues (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dini mbalimbali 
la Amani Tanzania (IRCPT), Rev. Canon Godda (wa pili kulia) wakishuhudi. 
Kamanda
 wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo 
(kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio 
hilo.
 Mgeni
 rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa 
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira 
Rodrigues akiweka sahihi kama shuhuda katika kupitisha Azimio hilo.
Msajili
 wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi naye akiweka saini kama
 shuhuda wa kupitisha Azimio hilo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa 
Mwanza, Baraka Konisaga.
Pichani
 juu na chini ni makundi ya Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini, 
Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Jeshi la 
Polisi na Walemavu waliodhuruia siku ya Kimataifa ya Amani Duniani 
ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Shule ya 
msingi Nyanza.
Wawakilishi wa vikundi vya vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.

Post a Comment