ARUSHA:WAFANYABIASHARA WAIOMBA SERIKALI IJAYO KUWA NA MFUMO MAALUM WA KUTATUA KERO ZAO
-->

Baadhi ya wafanyabiashara Jijini Arusha wameiomba serikali ijayo kutengeneza mfumo maalum utakaotatua kero mbalimbali zinazowakabili kwani wanashindwa kupata maendeleo kutokana na kukosa uongozi mzuri wenye kusikiliza na kutatua kero hizo.

Wakizungumza mapema leo wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali Jijini Arusha
ikiwemo Soko Kuu, Soko la Kilombero wameeleza kero zao ikiwemo kupatiwa
maeneo maalumu ya kufanyia biashara,kupewa mikopo yenye riba nafuu.
Blog hii imeshuhudia wafanya biashara wa mboga mboga, wakiwa wamepanga bidhaa zao chini,
ndani na nje ya stendi ya daladala Kilombero na kando ya barabara bila
kuchukuliwa hatua tofauti na ilivyokuwa miezi mitatu iliyopita ambapo askari
wa jiji walikuwa wanawakamata na kuwachulia bidhaa zao.
Post a Comment