MBEYA:WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA NA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)
|
Wito umetolewa kwa Waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na
maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na
kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo
ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri
ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Amesema ili
zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema
wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama
chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo.
Amesema mara
baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada
kusoma na kupitia vitabu vya maelekezo
waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa
zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu..
Baadhi
ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa
wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa
uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa
halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.
|
Afisa
TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa
maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa
mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na
Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG
|
Daniel
Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo
ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa
Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri
kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .
|
Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.
|
Post a Comment