MTANGAZAJI

UINGEREZA:MKUTANO WA UHURU WA DINI WAENDELEA HUKO MORTIMER READING


 

. Wajumbe wakifuatilia mada ya siku
Dr Kavaloh akidadavua mada ya mchana wa j'mosi, 30 Mei 2015
Tegemea Champanda katika mkutano

Na Tegemea Champanda,Uingereza
 'KUUJUA WAKATI' ni kichwa cha mada kuu inayo ongelewa hapa katika hoteli ya Devere iliyopo Wokefield Park, Goodboys Lane, Mortimer Reading, West Berkshire, Uingereza.  

Kanisa la waadventista wasabato katika British Union Conference, likizingatia wimbi la mambo na mageuzi mbali mbali yanayoendelea pande zote duniani, imeona vema liwanoe wakuu wa idara za Uhuru wa Dini na mahusiano ya kijamii makanisani kwa kuwaleta pamoja tangia Ijumaa ya 29 hadi J'pili ya 31 Mei 2015.

 Huu ni mkutano wa kwanza wa aina yake kufanyika kwa ajili ya idara hiyo unaojumuisha conferensi mbili zilizo katika union hii zikiwa ni ya Kaskazini na kusini kwa majina ya North England Conference na South England Conference. 

 Pamoja na kukumbushwa majukumu yao, viongozi wa idara ya Uhuru wa Dini na mahusiano ya kijamii wameendelea kusisitiziwa kwamba wao ni walinzi walio juu ya kuta za Sayuni (Isaya 21:11-12). Wanawajibu wa kuwalinda walio ndani ya kuta na makanisa mahalia  lakini pia wanapaswa kujua nini kinachoendelea nje ya kuta kwa maana ya mambo ya ki mataifa . 

 Wazungumzaji wanaendelea kutujuza tena kwa undani kwa yapi yanayojili na athari zake kwa kazi ya Mungu katika maeneo tunayoishi lakini pia na dunia nzima.

 Mch.Brighton Kavaloh ambaye ni mchungaji msaafu tokana na maradhi ya kiharusi yaliyo mkumba hivi karibuni, anakumbusha kwamba hatupaswi kuchukua mtazamo finyu wa yale yanayotokea duniani sasa. 

Kwa hivi licha ya kulifahamu neno la Mungu linavyotuelekeza lakini pia tunapaswa kuwa na ufahamu wa ki sheria kuhusiana na yale yanayogusa moja kwa moja uhuru wa dini.

 Wazungumzaji wengine wanao endelesha semina hizi ni pamoja na Ms Sonia Munroe ambaye ndiye mzungumzaji mkuu katika vipindi vya maombi ya asubuhi, Pr Cecil Perry, Mwenyekiti mstaafu wa British Union Conference, Pr Sam Davis mwenyekiti wa South England Conference, Pr Steve McKenzie muhubiri wa ibada mkuu pamoja na Pr Ian Sweeney mwenyekiti wa North England Conference. 

Ratiba zinasimamiwa na Paul Lee ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa Conference ya Kusini. 

Kuutambua wakati ni jukumu la kila muumini anayesubiria marejeo ya Yesu Kristo kwa mara ya pili. Tafadhari dumu kuiombea kazi ya Mungu duniani

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.