NAIROBI:RAIS UHURU KENYATTA ALISIFU KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO


![]() |
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato |

![]() |
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto (wa pili toka kulia)akifafanua jambo |


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelisifu Kanisa la
Waadventista Wa Sabato kwa namna linavyojihusisha katika kuboresha maisha barani Afrika na akachangia
dola 22,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 37 kwa
ajili ya ujenzi wa jengo la sayansi ya afya la Chuo Kikuu cha Afrika cha
Kiadventista kilichopo Ong’ata Rongai,Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza kwenye tukio hilo la kuchangia jengo hilo Rais
huyo amesema kuwa anafurahishwa na kazi zinazofanywa na kanisa hilo katika sekta za elimu na afya
kupitia taasisi zake zilizoko nchini Kenya.
Katika changizo hilo Chuo Kikuu cha Afrika cha Waadventista kilichoko karibu na yalipo Makao Makuu ya Kanisa hilo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kilifanikiwa
kukusanya shilingi milioni 50 za Kenya kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la sayansi ya afya .
Tukio hilo pia lilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa
Serikali ya Kenya akiwemo Makamu wa Rais William Ruto na pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika
Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati Dr Brasious Ruguri
Post a Comment