MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU: KUWAWEZESHA VIJANA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KIAFYA BARANI AFRIKA
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya
Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa
Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria
mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya
maamuzi sahihi ya kiafya
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller
(kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa
ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia
masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi
sahihi ya kiafya.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi
na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller wakati wa mkutano wa
kuzungumzia masuala ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya
maamuzi sahihi ya kiafya barani Afrika.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa
Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa mkutano wa kujadili
masuala ya masuala ya elimu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya
kiafya. Mkutano huo ni sehemu ya Maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa
Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa.
Baadhi
ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa
Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama
Salma Kikwete.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwa na wageni wengine mashuhuri wakifuatilia
kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa
kujadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika kuhusu kufanya maamuzi
sahihi ya kiafya ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani. Aliyekaa wa
kwanza kushoto ni Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi wa Ujerumani
Mheshimiwa Gerd Mueller akifuatiwa na Mama Getrude Mutharika na wa
kwanza kulia ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Masuala ya Vijana Bwana Ahmed Alhendawi.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais Malawi
Mama Getrude Mutharika mwishoni mwa mkutano wa kujadili masuala ya elimu
kwa vijana barani Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.
Aliyesimama katikati ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu
Tuvako Manongi.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sheila Tlou,
Mkurugenzi wa UNAIDS – Regional Support Team for Eastern and Southern
Africa na Waziri Mstaafu wa Afya wa Botswana na kushoto ni Mke wa Rais
wa Malawi Mama Getrude Mutharika mara baada ya kumalizika mkutano wa
siku moja uliofanyika huko New York hivi karibuni.
Chanzo: amani-mwaipajablog
Post a Comment