MOROGORO:KONFERENSI YA MASHARIKI MWA TANZANIA (ETC) YA WAADVENTISTA WASABATO SASA KUGAWANYWA
Tume ya Divisheni ya Africa Mashariki na Kati ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato leo imetangaza kuridhishwa na kuigawa konferensi
ya mashariki mwa Tanzania ETC kuwa koference mbili na kukipa hadhi Kiwanda cha
Uchapaji (TAP) kuwa nyumba ya uchapaji.
Mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania Mch Magulilo Mwakalonge amesema
kuwa tume imetathimini uwezekano wa kugawa ETC kuwa Konferensi mbili yaani konferensi ya Mashariki na Kati mwa
Tanzania na Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania na
TAP kupewa hadhi ya kuwa nyumba ya uchapaji.
Mchungaji Mwakalonge amesema kuwa kazi
iliyobaki ni tume kupeleka pendekezo na hati katika kamati ya division, na kinachosubiliwa
ni maamuzi ya kamati ya division ambapo hivi karibuni tume hiyo iliyokuja
kutoka nairobi yalipo makao makuu ya divisheni hiyo ilikuwa na wajumbe watano.
Post a Comment