MRADI WA VOLUNTEER TANZANIA WAJA
Mradi huu unaundwa ili kutatua matatizo makuu mawili:-
Kwanza: Ajira
Upande wa ajira ni kuwa vijana wengi wanamaliza shule
wakiwa hawana ujuzi wa kutosha wa shughuli za uzalishaji hata zile ambazo
wamesomea na kupata vyeti. Hivyo basi wanahitaji kupata fursa za
kujishughulisha hususani wakisaidiwa na wale wenye uzoefu ili waweze kupata
uzoefu utakaowawezesha kuwa imara katika kutafuta ajira katika soko gumu la
ajira.
Pili:
Shughuli za kimaendeleo
Upande wa shughuli za kimaendeleo ni kwamba zipo
shughuli nyingi za kimaendeleo zinakwama kwa sababu ya kukosa msukumo wa
kiutendaji kwakuwa hawajapatikana watendaji wenye ujuzi unaotakiwa kufanya
shughuli husika. Pia shughuli nyingi hukwama kwakuwa kuna rasilimali nyingine
zinahitajika ila ni ngumu kupatikana kama vile fedha na vifaa kwakuwa wenye
shughuli husika hawajawa na uwezo wa kutosha wa kifedha kununua vifaa husika,
au hawajawa na ujuzi wa kutosha wa kiutendaji, kimuundo n.k katika kujizalishia
rasilimali wanazozihitaji.
Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya hapa VoluteerTZ
Post a Comment