JAMII PRODUCTION YAZINDULIWA RASMI
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini Tanzania Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano mafupi aliyofanya na Jamii Production kabla ya KUZINDUA RASMI shughuli za kutayarisha na kusambaza matangazo ya Radio na Video.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara nchini Tanzania akiwa na waanzilishi wa Jamii Production, Mubelwa Bandio (kulia) na Abou Shatry (kushoto)
Naam....
Kwa baraka za Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara, JAMII RASMI IMEZINDULIWA RASMI Oktoba 26, 2013,
alipotutembelea kuangalia utendaji wetu na kuizindua rasmi hapa ofisini
kwetu Washington DC.
Hii ilikuwa ni ZAIDI YA TUKIO.
Ilikuwa ni BARAKA KWETU na tunamshukuru kila aliyewezesha hili.
NA SASA.....
Kazi ya kutekeleza yale yaliyousiwa na Mhe Waziri, yaliyo yaliyo msingi
wa kituo chetu, yale yaliyo MAHITAJI ya walaji (hadhira yetu) NA WAJIBU
WA FANI YETU ndio imeanza.
Na......
Hakuna litajalokuwa na maana kama hatutajua namna ambavyo utendaji wetu unaathiri maisha yako kwa namna CHANYA na HASI
Wewe (msikilizaji, mtazamaji na msomaji wetu) ni mdau mkubwa wa kufanikisha hili.
Tuzidi kushirikiana
TWAWAPENDA
Msimamizi wa vipindi na mpigapicha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry akisisitiza jambo kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA Georgina Lema akiwa "kitini"
Mmoja wa wawezeshaji wakuu wa Jamii Production Bwn Isidory Lyamuya wa Prestige Health Services akijaribu vitendea kazi vya kituo
Mhe. Waziri Mukangara akipokea maelezo ya utendaji wa kituo. Kushoto ni Afisa Ubalozi Mindi Kasiga
Mhe. Waziri akisikiliza RISALA ya Jamii Production
Mhe. Waziri Mukangara akijibu risala ya Jamii Production
Bwn Isidory Lyamuya akipata akipata picha ya pamoja na Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
>Bwn Isidory Lyamuya akipata mkono wa pongezi toka kwa Mhe. Waziri kwa msaada anaotoa kufanikisha kazi za Jamii Production
Abou Shatry akipongezwa na Mhe Waziri Mukangara
"Mwanamama" Georgina Lema wa kipindi cha FAMILIA akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
Mkurugenzi wa Mambo Jambo Radio Bwn Julius Makiri ambaye aliungana nasi katika uzinduzi huu rasmi akipata kumbukumbu na Mhe. Waziri
Mhe. Waziri Dkt Fenella Mukangara na Afisa Habari katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mindi Kasiga pamoja na wanaJAMII
Hakuna ZAWADI kubwa sawa na kilichofanyika. Na zawadi pekee tuliyonayo ni UPENDO. Ambao hauonyesheki wala haupimiki.
Lakini....tunapenda POPOTE UWAPO, UKUMBUKE SIKU YA LEO.
Na hivyo..twaomba KIKOMBE hiki kiwe kumbukumbu ya tukio hili kubwa kwetu
Abou Shatry akiwa mahala anapopatawala zaidi...
Post a Comment