MTANGAZAJI

TAARIFA YA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MANISPAA YA ILALA,DAR ES SALAAM-TANZANIA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Huduma za Afya ni moja ya huduma za Jamii zinazotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa mujibu wa sheria ilianzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania.

Huduma za Afya zinazotolewa zimegawanyika katika sehemu mbili (2) Afya Kinga na Afya Tiba. Kwa madhumuni ya Mkutano wetu wa leo tutazungumzia sehemu ya Afya Tiba ambayo inahusu huduma zinazotolewa katika Zahanati, Vituo vya Afya pamoja na Hospitalo,  lengo ni kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma ya Afya. Ili kuweza kujiletea
maendeleo sote tunaamini kuwa tuna hitaji Jamii yenye Afya bora.

Manispaa ya Ilala ina jumla ya Hospital-9, Vituo vya Afya-29 na Zahanati-179 za umma,binafsi na za majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Kutokana na Idadi hiyo ya Miundombinu ya Afya ni wazi kabisa imerahisisha upatikanaji wa huduma hii kwa Jamii.

Kupandishwa hadhi kwa Hospitali ya Amana kuwa Hospitali ya Mkoa ya rufaa kwa manispaa ya ilala ni kiashiria cha kukidhi vigezo vya utoaji huduma kwa ngazi ya mkoa.Vile vile Hospitali ya Amana ni miongoni mwa hospitali 3 za mikoa Tanzania zilizopata utambuzi wa kimataifa wa utoaji wa huduma bora za maabara.

Idadi ya wagonjwa wanaofika kwa siku kwa ajili ya huduma ni kati ya 1500 hadi 2000.

Mfano ulio wazi ni upande wa huduma za Uzazi. Hospital ya Amana inazalisha kina Mama kati ya 80-100 kwa siku. Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na uwezo wa Hospitali.

Hatua zilizochukuliwa Katika kutatua changamoto iliyoko Hospital ya Amana ni pamoja na Serikali kukipandisha hadhi Kituo cha Afya Mnazi Mmojakuwa Hospital. Hivyo tunaiomba Jamii kutumia Hospital ya Mnazi Mmoja ambayo inafikika kirahisi na huduma zinazotolewa katika Hospital hii ni za kuridhisha kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa vya kutolea Tiba.

Hatua nyingine ni Zahanati ya Pugu imepandishwa hadhi na kuwa Kituo cha Afya ambacho kina uwezo wa kulaza wagonjwa 60 kwa siku na  Manispaa kwa sasa inajenga chumba cha upasuaji. Zahanati ya Chanika nayo pia imepandishwa hadhi na kuwa Kituo cha Afya. Hatua hizi zimelenga kusogeza huduma ya Tiba katika maeneo yaliyo mbali na Mji. Manispaa imeweka huduma ya magari ya kubeba wagonjwa kwa ajili ya dharura zinazoweza kujitokeza katika maeneo  haya.

Tunacho kituo cha Afya Buguruni ambacho kinahudumia wagonjwa 300 hadi 600 kwa siku. Kituo hiki kinatoa huduma mbalimbali kama vile huduma ya mama na mototo, Ushauri Nasaha na Upimaji wa hiari wa Virusi vya Ukimwi,huduma ya kifua kikuu n.k.

Katika kuhudumia makundi maalum hususan Wazee Manispaa ya Ilala imetenga vyumba kwa ajili ya Wazee katika hospitali ya Amana,Mnazimmoja.

Yapo maradhi ambayo serikali yetu imejizatiti kupambana nayo kwa bidii zote magonjwa haya ni pamoja na Malaria na UKIMWI.

Katika kudhibiti ugonjwa wa Malaria Manispaa ya Ilalainaendelea na zoezi la kuua mbu na viluwiluwi vya Mbu katika Kata za Mchikichini, Ilala, Buguruni, Vingunguti,Kipawa, Kiwalani, Kariakoo, Gerezani, Jangwani,Upanga Mashariki, Upanga Magharibi, Kisutu, Kivukoni, Mchafukoge, Tabata, Kimanga, Segerea na Kinyerezi.

Ushauri unatolewa kwa Jamii kuhakikisha inaishi katika mazingira safi yanayozuia mazalia ya mbu waenezao malaria.

Huduma za Afya kwa wagonjwa wa UKIMWI na Kifua Kikuu zinatolewa katika Vituo vyote vya Afya, Zahanati na Hospital za Serikali na kwenye baadhi ya vituo binafsi.

Kwa ujumla mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma nya Afya kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 ni kama ifuatavyo;

Ø Zahanati zimeongezeka kutoka 17  hadi 25

Ø Idadi ya watumishi imeongezeka kutoka 1006-1312

Ø Kupandisha Hadhi Zahanati mbili(Chanika na Pugu) kuwa vituo vya Afya

Ø Ujenzi wa Jengo la kuhifadhi chanjo-Buguruni

Ø Ujenzi wa jengo la kutoa huduma za UKIMWI (Centre of Excelence0- katika Hospital ya Mnazi Mmoja

Ø Idadi ya Vituo vya Ushauri Nasaha kutoka 48 hadi 52

Mafanikio yaliyoanishwa hapo juu ni matokeo ya ushirikiano wa Wadau mbalimbali. Manispaa ya Ilala inatoa shukrani kwa Wafadhili mbalimbali, na Viongozi wote ambao wamekuwa wakielekeza misaada katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya.

Imeandaliwa na,

Tabu F.Shaibu

Afisa Uhusiano-Manispaa ya Ilala

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.