MWIMBAJI WA AMBASSADORS OF CHRIST YA RWANDA ACHUMBIWA TANZANIA NA MWIMBAJI
Warren Bright akimvisha pete ya uchumba Humure Rebecca |
Kutoka kushoto ni Humure Rebecca,Warren Bright na Nelson Manzi |
Mwimbaji wa Sauti ya kwanza wa Ambassadors of Christ ya Rwanda Humure Rebecca amechumbiwa na Mwimbaji na Kiongozi wa kundi la Voices of Victory la jijini Dar es salaam,Warren Bright,sherehe fupi ya uchumba ilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Warren Bright,Kunduchi jijini Dar es salaam Agosti 17,2013 na ilihudhuriwa na waimbaji baadhi ya mbalimbali wa nyimbo za injili nchini Tanzania na mwimbaji wa kiume wa Ambassadors of Christ,Nelson Manzi.
Warren ambaye ameweka picha za tukio hilo katika wasifu wake wa facebook amesema arusi yao inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Waimbaji wengine wa Ambassadors of Christ ambao wamefunga pingu za maisha na waimbaji wenzao ni Dushimimana Desire ambaye hivi karibuni alimuoa mwimbaji wa kwaya nyingine ya mjini Kigali na Umurisa Yvonne mwimbaji wa solo ya wimbo wa Kwetu Pazuri aliyeolewa na Josué Blaise Habimana aliyekuwa mwimbaji wa Halelujah Choir ya Gisenyi,Rwanda na kwa sasa wana mtoto mmoja wa kike.
Post a Comment