MTANGAZAJI

MWIMBAJI WA AMBASSADORS OF CHRIST YA RWANDA ACHUMBIWA TANZANIA NA MWIMBAJI


Photo: Thank you Lord
Warren Bright akimvisha pete ya uchumba Humure Rebecca
Photo: Manziiiiiiiiiiiii Ndagukunda cyaaaaaaaanee murumuna wanjye GOD BLESS YOU thank you for always being there for me.
Kutoka kushoto ni Humure Rebecca,Warren Bright na Nelson Manzi

Mwimbaji wa Sauti ya kwanza wa  Ambassadors of Christ ya Rwanda Humure Rebecca amechumbiwa na Mwimbaji na Kiongozi wa kundi la Voices of Victory la jijini Dar es salaam,Warren Bright,sherehe fupi ya uchumba ilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Warren Bright,Kunduchi  jijini Dar es salaam Agosti 17,2013 na ilihudhuriwa na waimbaji baadhi ya mbalimbali wa nyimbo za injili nchini Tanzania na mwimbaji wa kiume wa Ambassadors of Christ,Nelson Manzi.

Warren ambaye ameweka picha za tukio hilo katika wasifu wake wa facebook  amesema arusi yao  inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Waimbaji wengine wa Ambassadors of Christ ambao wamefunga pingu za maisha na waimbaji wenzao ni Dushimimana Desire ambaye hivi karibuni alimuoa mwimbaji wa kwaya nyingine ya mjini Kigali na Umurisa  Yvonne mwimbaji wa solo ya wimbo wa Kwetu Pazuri  aliyeolewa na Josué Blaise Habimana aliyekuwa mwimbaji wa Halelujah Choir ya Gisenyi,Rwanda na kwa sasa wana mtoto mmoja wa kike.

1 comment

Anonymous said...

Kila La heri WARREN AND Rebbeca. Mungu awajalie mema maishani.

Mtazamo News . Powered by Blogger.