MTANGAZAJI

MKUTANO WA MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI TANZANIA

IGP Said Mwema


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO WA MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI NCHINI


Jeshi la Polisi nchini linatarajia kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa maofisa wakuu waandamizi mjini Dodoma, utakaowashirikisha makamanda wote wa mikoa na vikosi kuanzia tarehe 12 Februari, 2013 hadi tarehe 15 Februari, 2013.


Lengo la mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo utekelezaji wa maazimio yaliyoafikiwa katika mkutano wa mwaka 2012 pamoja na kuweka mikakati ya namna ya kuendelea kudhibiti na kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini.


Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dk Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye atafungua rasmi mkutano huo siku ya Jumanne tarehe 12 Februari, 2013.


Katika mkutano huo, mada mbalimbali zitatolewa na wadau kutoka ndani na nje ya Jeshi la Polisi, mada hizo zitalenga kuimarisha uwezo wa namna ya kuzuia, kupambana na kutanzua uhalifu hapa nchini. Aidha,  namna ya kuendelea kuishirikisha jamii katika  mapambano dhidi ya uhalifu kuanzia ngazi ya familia.


Mkutano huo pia, unatarajiwa kuhudhuriwa na mawaziri mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Waziri wa Fedha, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Waziri wa Kazi na Ajira, Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Kilito, Chakula na Ushirika, Waziri wa Ardhi na Makazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mifugo na Uvuvi pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.


Kauli mbiu katika mkutano huo ni “Tujenge uwezo wa Jamii na Polisi katika kukabiliana na Vurugu kwa kuimarisha Utii wa Sheria bila Shuruti”.


Imetolewa na:
Advera Senso
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T),
Makao Makuu ya Polisi.
10 Februri, 2013.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.