MTANGAZAJI

WANAWAKE WANAONGOZA KUWAPIGA WAUME ZAO DAR


Balozi wa Sweden nchini Tanzania Lennarth Hjelmaker akitoa hotuba wakati wa Unzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya Mwaka 2011
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba akizindua rasmi ripoti hiyoWatu waliokuwepo kwenye uzinduzi huo

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimezindua Ripoti yake ya Haki za Binadamu ya mwaka 2011 inayoonyesha pamoja na mambo mengine, wanawake visiwani Zanzibar na katika Mkoa wa Dar es Salaam, wanaongoza kuwapiga waume zao.

Mbali na ukatili huo kwa wanandoa, ripoti hiyo imeonyesha pia kuwa vitendo vya rushwa nchini vimeendelea kuwa sugu na kugusa maeneo muhimu kwa ustawi wa jamii, ikiwamo bungeni ambako imedai kuwa baadhi ya wabunge wanahongwa ili kupitisha bajeti za wizara.

Akisoma ripoti hiyo katika hafla ya uzinduzi wake uliofanyika Dar es Salaam mei 28 mwaka huu,Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema asilimia 7.3 ya wanawake wa Unguja Kusini huwapiga waume zao wakifuatiwa na Mikoa ya Dar es Salaam, Mjini Magharibi na Lindi ambako asilimia 5.3 ya wanawake huwapiga waume zao.

“Hata hivyo, Dar es Salaam inashika nafasi ya pili kwa kuwa ina watu wengi ikilinganishwa na mikoa mingine. Mkoa wa mwisho ni Iringa ambako tatizo hilo liko kwa asilimia 4.7,” alisema.  Dk Bisimba alisema ripoti hiyo ni ya 10 kuzinduliwa na LHRC na ya mwaka huu imegusa maeneo mbalimbali na kuanisha yale ambayo haki za binadamu zinakiukwa kwa kiwango kikubwa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.