MTANGAZAJI

MAJAMBAZI WATEKA BASI KIBONDO KATIBU UVCCM AUAWA

Basi la Kampuni ya China ya Golden Intercity Express lenye namba za usajili T 457 ARC lilikuwa limebeba abiria 51 lilitekwa na Majambazi leo katika eneo la Mkugwa wilayani Kibondo, inasemekana majambazi hao walipiga sana Risasi, akielezea Mkasa huo kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, mmoja wa Wasafiri aliyekuwa ndani ya Basi hilo kutoka Kigoma kwenda Mwanza, Sophia Nasibu alieleza kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi ambapo alishuhudia Majambazi yakipiga risasi ovyo kwenye Basi hilo na hivyo Dereva kulazimika kusimama porini hapo.

Katika kufyatua risasi inasemekana wameweza kumuua Willy Muga katibu wa UVCCM mkoani Mara. Aidha Sophia ameeleza kuwa majambazi hao yalikuwa yakipiga kelele kuwaamrisha Askari wawili wanaosindikiza Basi letu wasalimishe Bunduki zao, na baada ya muda mrefu huku yakitupiga risasi kutoboa toboa basi ndipo Askari hao wanaosindikiza Basi waliogopa na kuamua kusalimisha Bunduki zote mbili walizokuwa nazo, walizitupa mlangoni na Majambazi yakazichukua.


Majambazi hayo baada ya kuchukua Bunduki za Askari hao yalipoanza kuwapora Abiria fedha walizokuwa nazo huku wakiwachapa viboko baadhi ya waliokuwa wakorofi na ambao walionekana kukaidi.Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, George Mayunga alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema kwamba amepata taarifa lakini bado anasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Kamanda wa Polisi wilayani Kibondo (OCD) Innocent ili aweze kuandaa taarifa rasmi.

Na:Frederick  Katulanda

1 comment

sophoni ndahiyimbaze said...

wakishikwa watiwe gerezania
tumeshiba kusikia eti watu waibiwa
i never sleep or night becouse of them. when i was in nduta we all ways stay outside to guided them because of their atittude.

Mtazamo News . Powered by Blogger.