MTANGAZAJI

UNAMLINDA MWANAO NA MTANDAO?

Ni miaka 3 iliyopita ambapo vijana 5 wa kimarekani walianzakuwasiliana na mtu waliyekutana nae kwenye mtandao wa facebook.com kwakuwa rafiki huyo mpya alikuwa na nia ya kupata vijana wengi zaidi kwaajili ya shuguli zao basi akajificha chini ya profile inayowapendezavijana wale .

Aliweka picha nzuri ya kijana wa kipakistani lakini mwenye uchu wakwenda kusaidia wenzake nchini Afghanistan na nchi zingine ambazoinaonekana ni maadui zao ,wale vijana wakapenda yote haya kupitiamtandao wa facebook.comBaada ya kujuana kwa kipindi kirefu rafiki wa facebook.com akawaalikavijana wale 5 kwenda Pakistan huko Pakistan kwenye mpaka wake naAfghanistan kwenye nyumba moja kuna watu usiku wataenda kuwachukuwa .

Ilikuwa ni bahati nzuri vyombo vya usalama vya nchi hiyo ya Pakistanviliweza kugundua mbinu hii vijana walikamatwa na sasa hiviwamefunguliwa mashitka huko Pakistan kwenye gereza la kijeshi kifungochake kinaweza kuwa cha maisha endapo watapatikana na makosa .

Lakini inawezekana pia kwamba hawa vijana walikuwa wanatumiwa navyombo vya usalama vya kimarekani kwa ajili ya kwenda kufanya kazinchini aghanistan kwa kujua au kutokujua .Na kama umesoma vyombo vya habari kwa siku za karibuni lazima utakuwaulisoma habari za kijana mmoja wa kitanzania kuuwawa mitaani kwasababu aliweka ujumbe kwenye profile ya mwenzake ambaye nae alikuwamwanachama wa facebook.com hiyo ilikuwa ni ulayaHapa nyumbani Tanzania vijana wengi sana wako kwenye mitandao hii ya
facebook hi5 na hata twitter huko wanakutana na marafiki na watuwengine mbalimbali , kwakuwa sisi watanzania tunajulikana ni watuwapole , watu wa amani na utulivu basi wale wenzetu wa afrika yamagharibi wanatumia upole , utulivu huu kufanya uhalifu wa ainambalimbali .


Nadhani umewahi kusoma sehemu kuhusu watu mbalimbali wanaopatamatangazo ya nafasi za kazi kwenye anuani zao za barua pepe wanapojibutu kuanzia hapo ndio huwa wamepata nafasi ya kwenda kufanya kazi kubwakubwa huko nje si ndio ?Watu wengi wameenda kuuzwa kwenye nchi za watu kama machangudoa namashoga saa zingine na watanzania wenzao kwa kukutana kwenye mitandaohii wengine wametumika katika kusafirisha madawa ya kulevya kwenyenchi za watu haswa afrika ya kusini na asia , wengine ni wapiganajikwenye vikundi vya kigaidi kama huko uarabuni na Somalia .

Pamoja na yote hayo hata hivyo mitandao hii inaweza kutumika kwa faidavile vile ingawa kwenye faida ni lazima mtu Fulani akose , tubakiekujua tu kwamba mitandao ya jamii kama facebook.com hi5 na twitter niaina mpya ya starehe na burudani lakini ambayo hapo hapo kuna ubaya nainaweza kukuletea matatizo makubwa sana ni shauri yako wewe kuamuakucheza karata zako vizuri kwa wazazi wafuatilie watoto wao kujuawanaowasiliana nao kwa njia ya mtandao haswa kwenye hizo facebook nawale wanaowafuatilia kutumia twitter na mitandao mengine mengi tuambayo mtu anaweza kuweka picha na taarifa zake zingine .

Na kwa kumalizia ni vizuri kujua kwamba matukio mengi yanayohusiana naugaidi kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita yameanzia au kuendelezwamawasiliano yake kupitia mitandao ya jamii haswa facebook.comMfano kuna Yule askari ambaye aliyewa na asili ya Lebanon yeye
alitumika kama chambo kuingilia mitandao ya magaidi huko Afghanistanna majasusi wa magaribi lakini hapo hapo kumbe alikuwa anatumika namagaidi hao hao .Ilibaki dakika chache majasusi hao wakamkamate ili aweze kuhojiwakwenye kambi moja huko Afghanistan kwa sababu aliingia sehemu ambayosio yake na ndipo hapo alipojilipua na kuuwa wenzake kama 6 hivi ambaoni maofisa usalama wa kimarekani simulizi hii inafanana na hiyo yajuu ya hao vijana 5 waliokamatwa Pakistan .


Walivyofuatilia iligundulika kwamba aliwahi kuandika ujumbe kwenyemtandao mmoja wa jamii na kusisitiza nia yake ya kulipiza kisasi kwamauaji kama ilivyotokea hapo juu .Hata Yule kijana wa Kinigeria aliyekamatwa ndani ya ndege wakati wamkesha wa xmass nchini marekani nae alipochunguzwa alikutwa kumbealiwahi kuandika pamoja na kuhimiza vijana kujiunga na magenge yakigaidi ulimwenguni utaweza kuona ujumbe huo kwenye tovuti mbalimbaliza kinaigeria .

Kuanzia hapo wazazi wa kinigeria kwa mamia wamekuwa wakiwasiliana nawatoto wao mara kwa mara haswa wale waliokuwa nje ya nchi hiyo nakuanza kujua taarifa na kile wanachokifanya wasije kuwa kina muttalab wengine .

Mdau Yona Phares Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.