MBWA ANAPOKUA KITOWEO!!!!!!
Mkazi wa Kihesa katika manispaa ya Iringa akiendelea kumchuna ngozi mbwa aliyekuwa amegongwa na gari kwa ajili ya kwenda kumla kama kitoweo.
Tukio hilo la aina yake litokea majira ya jana saa 6 mchana katika eneo la kihesa Sokoni katika Manispaa ya Iringa ambapo mbwa huyo alikuwa amegongwa katikati ya barabara ya Kihesa Tumaini Iringa .
Kutokana na mzoga huu wa mbwa kubaki katikati ya barabara mkazi huyo ambaye alikuwa akinywa pombe ya kienyeji katika kilabu kimoja kilichopo jirani na eneo hilo alilazimika kunoa kisu chake na kumsogea mbwa huyo pembeni ya barabara na kuanza kumchuna ngozi huku akionyesha kuchekelea kuwa amepata mboga.
Kwa maelezo zaidi bofya hapa http://francisgodwin.blogspot.com/
Post a Comment