MTANGAZAJI

DU!!! BIKIRA INAPOUZWA!!!!! DUNIANI KUNA MAMBO


Hatimaye Bikira Yake Yanunuliwa Kwa Euro10,000

Yule msichana wa Romania aliyatangaza kuiweka bikirayake kwenye mnada nchini Ujerumani miezi michache iliyopita amefanikiwa kupata mtejabaada ya mnada huo kuisha na mwanaume mmoja raia wa Italia kufikia dau la euro10,000.

Alina Percea mwenye umri wa miaka 18 aliinadi bikira yake kwenye tovuti moja nchini Ujerumani miezi michache iliyopita.Alina alipanga kuzitumia fedha atakazopata baada ya kuuza bikira yake kwaajili ya kujisomeshea chuo kikuu na kuisaidia familia yake masikini iliyopo nchini Romania.

Mnada huo ulifikia tamati siku ya alhamisi kwa Muitaliano mmoja ambaye hakutajwa jina lake kuibuka mshindi katika dakika za mwisho mwisho za mnada huo. "Nasubiri kwa hamu, nilifikiri dau lingepanda juu zaidi lakini hata hivyo nina furaha" alisema Alina.

Alina aliwasili Mannheim, Ujerumani mwezi januariakitokea kwao Romania na aliamua kuingia kwenye mnada huo baada ya kushindwa kupata kazi.Mnada huo uliingia dosari wiki tatu zilizopita baada ya mwalimu wa shule ya zamani ya Alina kudai kuwa Alina sio bikira.

Hali hiyo ilipelekea Alina ambaye kabla ya mnada huo alipimwa bikira yake, ilimbidi afanyiwe majaribio kwa mara ya pili kuthibitisha bikira yake. Daktari aliyemfanyia majaribio hayo alitangaza katika kikao na waandishi wa habari kwamba "Alina kweli ni bikira na hajawahi kufanya mapenzi".

Alina aliamua kuinadi bikira yake baada ya kuonamafanikio aliyoyapata mwanafunzi wa Marekani Natalie Dylan mwenye umri wa miaka 22ambaye alipata mteja wa bikira yake aliyoinadi kwenye tovuti moja nchini humo aliyefikia dau la dola milioni 3.5.

" Hakuna mtu aliyeniambia nifanye hivi, nimatakwa yangu binafsi" alisema Alina. "Sijui ni lini au wapi nitakutana na mshindi wangu, lakini nafurahia kusafiri iwapo atalipia gharama za usafiri".

"Tutaenda hotelini katika wiki chache zijazo na tutatumia usiku mmoja pamoja, na kama tukipendana tunaweza tukakaa pamoja na usiku wa pili". "Tunaweza tukatumia kondomu au kama atafanyiwa vipimo vya magonjwa ya zinaa niko tayari kumeza vidonge vya kuzuia mimba".

"Natumaini jamaa ataelewa kuwa mimi ni bikirahivyo atanihudumia vizuri" alimalizia kusema Alina.

5 comments

Anonymous said...

du! kumbe biashara ni matangazo nilikuwa sielewi lakini dunia ya sasa kuna mabikira wachache ambao pia hawapendi kujitangaza kama vile watu wenye virusi vya ukimwi

lakini nafikiri huyu dada ameamua kubikiriwa kwa sababu ya umasikini wake lakini ipo siko ambayo atajuta kwa kuuza ubikira wake kwa pesa na kwa mtu ambaye atakuwa siyo mume wake

Anonymous said...

Jamani wadau hii ni halali kweli kuuza bikira pamoja na kubanwa sana na hali ya maisha? Kwa kweli huyu bindi ana malengo mazuri lakini ametumia njia isiyo sahihi.Lakini nampongeza kwa kujitahidi hadi amempata mteja na kupata euro 10,000.Lakini sasa hajui jamaa atakavyo mfanyia sijui kama atamfanya kwa hasira ya pesa zake ATAJIJU MWENYEWEEEEEEEEEEE!

Yasinta Ngonyani said...

Jamani sasa dunia imeharibika watu wanathubutu hadi kuuza ubiira na watu wananunua. kazi kwelikweli. lakini kwa nini asiolewwe tu, ina maana anaona pesa ni muhimu sana kuliko mwili wake ndio najua hana uwezo wa kusoma na kuisaidia familia yake lakini kuna njia nyingi za kutafuta pesa.

Jr said...

kazi ipo, laana tupu

Unknown said...

Ni upuuzi, ushetani,wote wawili wanapaswa kuokoka na kuacha dhambi maana hukumu yao itakuwa kubwa kama wasipo tubu

Mtazamo News . Powered by Blogger.