MTANGAZAJI

MATUNDA

Ndizi mbivu zikiuzwa sokoni Morogoro

Mkoa wa Morogoro unasifika kwa kuwa na aina mbalimbali za matunda kwa kipindi cha mwaka mzima hii ikiwa na maana kwamba ukienda katika soko kuu la Morogoro na kwenye masoko madogomadogo utakuta matunda tofauti tofauti kwa kila mwezi.

Matunda kama vile ndizi,machungwa,mapalachichi,matikiti,maembe,matunda damu,mafenesi,machenza n.k ambayo hutoka hasa sehemu mbalimbali za mkoa huu kama vile Mgeta,Mlali,Matombo,Kisaki n.k cha kushangaza ni kwamba matunda mengi hayapati soko la uhakika na mengi huozea shambani,yanaposafirishwa ama sokoni kwa kuwa miundo mbinu ni mibovu na pia hakuna soko la uhakika.Kwani wakulima wengi hutegemea soko la hapa Morogoro mjini ama huko Dar es salaam ambako nako hununuliwa kwa bei ya "kutupwa"na walanguzi.

Hivi karibuni kuna taarifa kwamba kuna kiwanda cha kutengeneza juice kilichopo Morogoro ingawa hata hivyo sijaona ama kusikia kinawanufaisha vipi wakulima wa matunda haya na kunusuru hali ya utajiri wa matunda uliopo Morogoro jambo ambalo nchi zingine zilizoendelea lingekuwa jambo la kujivunia na kuwasaidia wananchi wa mkoa huu kupiga hatua mbele katika maendeleo kila kukicha tunapewa "hadithi za alinacha" na "tuliowapa kura za kula"

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.