MTANGAZAJI

JAMII YETU

Ni saa 10.40 jioni kwa saa za hapa nchini nikiwa natangaza kipindi cha JAMII YETU ambacho kiko mbashara( live) kuanzia saa 10 jioni hapa Morning star 105.3 fm,Mikocheni B,katika jiji la Dar es salaam,wasikilizaji wengi wameshatoa maoni yao kuhusu mada ya uamuzi wa kujiua mtu anapopatwa na matatizo katika maisha.

Nikiwa natumia namba ya simu ya ofisi nasikia sauti ya dada mmoja ikiwa hewani sauti ambayo iliashiria kuna jambo kutokana na jinsi ilivyokuwa ikisikika"NASHUKURU SANA KWA KIPINDI CHA LEO MAANA NILIKUWA NIMEAMUA KUJIUA KUTOKANA NA MATATIZO NILIYONAYO LAKINI BAADA YA KUSIKILIZA KIPINDI CHA LEO SINTOJIUA"Alimaliza kueleza na kukata simu dada huyu anayeishi hapa jijini.

Tangu nianze kutangaza kipindi hiki hapa Morning Star nimekuwa nikijifunza mambo mengi kutoka kwa wasikilizaji kuwa watu wanamatatizo ambayo yanahitaji msaada wa mawazo na ushauri mbalimbali na hivyo redio ni njia mojawapo ya muhimu sana katika hili na katika kuwapatia matumaini maishani mwao.

Ama kwa hakika sauti ya matumaini inahitaji kuwapatia matumaini wasio na matumaini katika kutumaini wanachopaswa kukitumainia

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.