WANAFUNZI WA BUGEMA WASHINDA MASHINDANO YA DUNIA ITALIA.
Wanariadha kutoka Chuo Kikuu cha Bugema, kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Uganda, wameibuka na ushindi mkubwa katika mashindano ya nyika ya vyuo vikuu duniani (FISU2026) yaliyofanyika Cassino, Italia hivi karibuni.
Mashindano hayo ya mbio ndefu yalikusanya wanamichezo bora wa vyuo vikuu kutoka zaidi ya nchi 30 duniani, yakionyesha kiwango cha juu cha mbio za umbali mrefu kwa wanariadha wenye viwango bora wanaosoma vyuo vikuu.
Yeko Elisha, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Bugema, alishinda medali ya dhahabu katika mbio za wanaume za kilomita 10 kwa muda wa dakika 30:27. Mshiriki wake wa timu, Solomon Cherotwo, alimaliza nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba, huku Hiromichi Nonaka wa Japan akishinda nafasi ya pili na medali ya fedha.
Ushindi huu wa juu ni wakati muhimu kwa Chuo Kikuu cha Bugema na kwa Uganda kwa ujumla. Unaonyesha jinsi chuo kinavyoimarisha jukumu lake katika kukuza wanamichezo wenye vipaji na pia kuongeza sifa ya Uganda katika mbio za umbali mrefu.
Mashindano ya hayo yalizinduliwa rasmi mwaka 1978 huko Lausanne, Uswisi na hufanyika kila baada ya miaka miwili ingawa mwaka 2020 yalisitishwa kutokana na janga la Uviko‑19. kabla ya mwaka 2026, mashindano hayo yamefanyika angalau mara zaidi ya 20 tangu kwanza kuanzishwa rasmi.
Mwaka 2024, Seth Akampa kutoka Uganda alishinda medali ya dhahabu katika FISU kwa mbio za kilomita 10 ambapo mashindano hayo yalifanyika Muscat, Oman.

.png)
Post a Comment