ZANZIBAR KUANZA USAFIRI WA MABASI YA UMEME
Usafiri wa umma wa
kutumia mabasi yanayotumia nishati ya umeme Zanzibar unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi
Februari, 2026, ukianzia Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Mradi huu unaotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unalenga kupunguza msongamano barabarani, kuboresha uhakika wa safari, na kuimarisha usafiri rafiki kwa mazingira.
Serikali kupitia kupitia ZSSF imeingia mkataba na Kampuni ya GRT Limited katika utekelezaji wa mradi huu, utakaotumia vituo vya kisasa na mfumo maalum wa uendeshaji katika barabara za kawaida.
Mradi huu utafanyika kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza itaanza Mkoa wa Mjini Magharibi kwa njia za,
Uwanja wa Ndege kwenda Malindi, Buyu - Chukwani – Mnazi Mmoja – Malindi.
Kituo cha Kijangwani kitatakuwa ni kiunganishi kikuu cha mabasi yote, sambamba na kuwepo kwa vituo ndani ya Uwanja wa Ndege na Bandari ya Malindi.
Mabasi ya umeme yanatarajiwa kuanza kuwasili mwanzoni mwa Februari mwaka huu.

.png)
Post a Comment