UTAWALA WA DONALD TRUMP WATANGAZA KUTOSHEREKEA MAADHIMISHO YA USHOGA
Utawala wa Donald Trump umetangaza kuwa hautasherehekea mwezi huu kwa maadhimisho ya kutambua ushoga.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, anasema juma hili kuwa “Rais wa sasa anajivunia kuwa rais wa Wamarekani wote, bila kujali rangi, dini, au imani."
Wanachama wengine wa Chama cha Republican wamependekeza hatua zaidi. Mwakilishi wa bunge Mary Miller amewasilisha azimio la kutangaza mwezi wa Juni kuwa Mwezi wa Familia, ikiwa ni juhudi za kudai tena mwezi wa Juni kwa ajili ya familia ya msingi (nuclear family).
Azimio hilo linaonya maadhimisho hayo kwa kuyaita “ya kupotoka,” ikiwezekana likimaanisha mavazi na mienendo ya kimahaba inayoshuhudiwa katika baadhi ya matukio ya mwezi juni.
Akizungumza na Daily Wire, Miller anasema, "Familia ya Kimarekani inashambuliwa kwa kasi na ajenda kali za mrengo wa kushoto ambazo zinajaribu kufuta ukweli, kufasiri upya ndoa, na kuwachanganya watoto wetu."
Aliendelea kusema, “Kwa kuitambua Juni kama Mwezi wa Familia, tunapinga uongo wa ‘Pride’ na badala yake tunaheshimu mpango wa Mungu usio na kasoro na wa milele huku akieleza kuwa "ikiwa tunataka kweli kuurejesha taifa letu, lazima tusimame kwa umoja kulinda na kuimarisha msingi uliolitengeneza familia.”
Pendekezo lake limeungwa mkono na mashirika kadhaa yanayojihusisha na masuala ya familia, yakiwemo Moms for America, American Family Project, na Family Research Council.
Uamuzi wa utawala wa Trump kuupuuza Mwezi wa Pride unatofautiana na msimamo aliokuwa nao katika muhula wake wa kwanza madarakani.
Mnamo mwaka 2019, Rais Trump alitumia mwezi wa Pride kutangaza kampeni ya kimataifa ya kutokomeza uhalifu dhidi ya ushoga duniani kote.
Katika muhula wake wa pili, moja ya hatua za kwanza za Trump ilikuwa kutoa amri ya kiutendaji inayothibitisha kuwa Marekani inatambua jinsia mbili tu ya kiume na ya kike.
Post a Comment