CHINA YATANGAZA SHERIA MPYA ZINAZOMINYA UKRISTO
Katika hatua iliyozua wasiwasi miongoni mwa watetezi wa uhuru wa Dini Duniani kote, China imetekeleza kanuni mpya zinazozidi kuzuia uhuru wa kuabudu, hasa kwa kuwapiga marufuku wamisionari wa Kikristo wa kigeni kushiriki katika shughuli za Kikristo ikiwemo kuhubiri na kutoa mafunzo. Pia, hivi karibuni imewateua maaskofu wawili wa Kikatoliki bila idhini ya Vatican.
Kanuni zilizorekebishwa hivi karibuni, "Sheria za Utekelezaji za Usimamizi wa Shughuli za Kidini za Wageni", zimeanzisha vikwazo vikubwa dhidi ya ushiriki wa wageni katika ibada za Kikristo, elimu, na shughuli za misaada ya kidini.
Sheria hizo zinakataza wageni kuhubiri, kusambaza vifaa vya kidini zaidi ya matumizi binafsi, au kushiriki katika shughuli zozote za imani bila idhini ya serikali mapema.
Wamisionari wa kigeni pia wamepigwa marufuku kuandaa masomo ya Biblia, kuchangisha fedha, au hata kutumia majukwaa ya mtandaoni kwa madhumuni ya kidini bila kibali rasmi kutoka kwa mamlaka.
Raia wa China pia wamezuiwa kushiriki katika shughuli kama hizo zinazoongozwa na wageni au kupokea msaada wa kidini kutoka kwa mashirika ya Kikristo ya nje ya nchi.
Wageni watakaokiuka masharti haya mapya ya kidini nchini China wako katika hatari ya kutozwa faini, kufukuzwa nchini humo au kushtakiwa.
Hata matukio halali ya kidini lazima yapitie njia rasmi za serikali, ingawa vibali vichache sana hutolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Open Doors, Henrietta Blyth,anasema .
Sheria hizi kimsingi zinahalalisha ukandamizaji wa aina nyingi za ushuhuda wa Kikristo na kazi za umisionari wa kigeni nchini China.”
Shirika la Open Doors la Uingereza na Ireland, linalojihusisha na utetezi wa wakristo kwa msaada wa vitendo na wa kiroho, limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuingilia kwa serikali ya China Kanisa Katoliki, jambo linalozidisha mvutano uliopo kati ya Beijing na Vatican.
Bila kuzingatia hitaji la idhini ya Papa, serikali ya China hivi karibuni iliwateua Joseph Huang Bingzhang na Anthony Xu Jiwei kuwa maaskofu wa Kikatoliki.
Uamuzi huo wa upande mmoja ulifanyika muda mfupi baada ya kifo cha Papa Francis, na kusababisha mashaka kimataifa na kuweka shakani makubaliano ya mwaka 2018 kati ya Vatican na China yaliyolenga kudhibiti uteuzi wa maaskofu kwa ushirikiano.
Wachambuzi wanaona hatua hiyo kama mkakati wa kisiasa wa kuonyesha mamlaka.
Ndani ya nchi, hali kwa Wakristo wa China imekuwa ikidorora kwa muda chini ya uongozi wa Xi Jinping. Serikali inakuza makanisa ya kizalendo yanayoendana na sera za dola, huku ikikandamiza makanisa ya nyumbani; mashambulizi, kukamatwa, na udhibiti mkali wa taarifa vimekuwa jambo la kawaida. Usambazaji wa Biblia pia unafuatiliwa kwa karibu.
China inashika nafasi ya 19 kwenye Orodha ya Dunia ya Open Doors 2024, inayotambua maeneo hatari zaidi kwa maisha ya Kikristo.
Kwa kujibu, Open Doors inahimiza serikali ya Uingereza na jumuiya ya kimataifa kushiriki kidiplomasia na kuiwekea Beijing shinikizo kuheshimu uhuru wa kidini.
Post a Comment