MTANGAZAJI

ENEO LINALOONGOZA KWA VIWANGO VYA DINI DUNIANI

 


Matokeo ya Utafiti wa mwaka 2023 kutoka Kituo cha Utafiti cha PEW umebaini kuwa Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara ina viwango vya juu zaidi vya uthamini wa dini duniani, huku angalau asilimia 90 ya watu wazima nchini Senegal, Mali, Tanzania, Guinea-Bissau, Rwanda na Zambia wakisema dini ni muhimu sana katika maisha yao.

Kinyume chake, Ulaya ina viwango vya chini, ambapo katika nchi kama Estonia, Jamhuri ya Czech, Uswisi, na Uingereza, ni asilimia 10 au chini ya hapo wanaosema hivyo.

Katika Asia ya Kusini na Kusini-Mashariki, hali si thabiti. Indonesia ina karibu watu wazima wote wakithamini sana dini, lakini ni asilimia 36 tu nchini Singapore na asilimia 26 nchini Vietnam wanaosema hivyo.

Marekani iko chini ya wastani wa dunia wa asilimia 55, ikiwa na asilimia 42 ya watu wazima wanaosema dini ni muhimu sana. Kwa maombi ya kila siku, Marekani iko karibu na wastani wa kimataifa wa asilimia 46, kwa kuwa asilimia 45 ya Wamarekani walisema huomba kila siku.

Katika Amerika ya Kusini, maombi ya kila siku ni ya kiwango cha juu: asilimia 82 nchini Guatemala na Paraguay, na asilimia 78 nchini Costa Rica na Honduras. Asia ya Mashariki ina viwango vya chini, ikiwa na asilimia 13 tu Hong Kong na asilimia 19 Japani.

Licha ya ibada za kidini kuwa chini, watu wengi katika Asia ya Mashariki wanaamini katika nguvu za kiroho na hushiriki kwenye mila kama kuwaenzi mababu. Utafiti huu pia ulitekelezwa kwa kina nchini Japani na Taiwan.

India ilionyesha kuwa dini inaathiri maisha ya kila siku, hasa kwa Wajain. Asilimia 92 ya Wajain hula mboga tu, na asilimia 67 hawali mboga za mizizi. Ni nusu tu ya watu wazima waliokubali kula katika nyumba ya mtu wa dini tofauti.

PEW inapanga kufanya tafiti mpya katika zaidi ya nchi 30 kwa wakati mmoja ili kupata uelewa wa kulinganisha kimataifa. 


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.