MTANGAZAJI

DIASPORA WA KENYA WANAVYOINUFAISHA NCHI YAO

 


Wakenya wanaoishi na kufanya kazi nje ya Kenya  walituma nyumbani pesa za Kenya sh Bilioni 39.9  sawa na Dola za Kimarekani milioni 339.7 mwezi wa Mei mwaka huu.

Pesa zinazotumwa na Diaspora wa Kenya zilikuwa asilimia 7.6 zaidi ya shilingi za Kenya Bilioni 37.1 yaani  Dola milioni 315.8 zilizotumwa nchini humo  kwa wakati kama huo mwaka 2021 kwa mujibu wa data kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK).

Utumwaji wa pesa hizo ni mwendelezo ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 41.7 za Kenya sawa na dola milioni 355 za Marekani  zilizotumwa nchini Kenya  Aprili 2022.

Taarifa ya benki ya akiba iliyochapishwa hivi karibuni  imeeleza kuwa Uingiaji mkubwa wa utumaji pesa unaendelea kusaidia akaunti ya sasa na uthabiti wa kiwango cha ubadilishaji nchini humo.

Marekani inasalia kuwa chanzo kikubwa zaidi cha kutuma pesa nchini Kenya ikichangia asilimia 57 ya mapato mwezi Mei.

Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka  2022, jumla ya pesa zilizotumwa nchini Kenya  na diaspora zinafikia shilingi  bilioni 201.8 ambazo ni sawa na Dola za kimarekani bilioni  1.719

Hii inawakilisha kiwango cha ukuaji cha asilimia 19 kutoka kwa kiasi cha shlingi bilioni .169.6 ama Dola bilioni 1.445 zilizotumwa Kenya na Diaspora  katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2021.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.