MTANGAZAJI

WAADVENTISTA NA MKAKATI WA MAOMBI YA FAMILIA

 


Kanisa la Waadventista wa Sabato kupitia Kikao cha Kamati Kuu ya Utendaji ya Kanisa hilo Duniani kilichomalizika hivi karibuni, limetangaza mikakati ya umuhimu wa ibada zinazowahusisha wanafamilia ili  kusaidia vijana wa Kanisa hilo kushikamana na Kristo.
Japokuwa karibu 50% ya Waadventista waliohojiwa mwaka wa 2018 hawana ibada za kila siku, na ni 34% tu ya familia zinazofanya ibada ya familia pamoja.
Konferenzi kuu ya Kanisa hlo (GC) imetangaza mpango wa kukabiliana na hali hii. 
Mojawapo ya malengo hayo ni mpango mkakati uliopewa jina la kauli mbiu ya  “Rudi Madhabahuni” ili  kuongeza maradufu idadi ya familia zinazofanya ibada pamoja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mpango wa huo wa kurasa 15, unaangazia malengo 18, kuanzia uundaji wa rasilimali mpya hadi kuhimiza uongozi zaidi kushiriki uzoefu wao wa ibada ya kibinafsi.
Mtazamo wa vyombo vya habari wa mpango huo ulikuwa wa kuvutia. Kwa upande mmoja, kuelimisha watu kuhusu "athari mbaya" ya vyombo vya habari vya kielektroniki na Kwa upande mwingine, malengo saba kati ya mengine yanahusisha matumizi ya mitandao ya kijamii na uundaji wa rasilimali za kielektroniki.
Nyenzo zingine ni pamoja na podikasti ya kila juma, programu ya ibada kupitia vitabu vya Mama Ellen G White, mfululizo wa video kuhusu Nyumba ya Kiadventista na Kanzi data ya Mapendekezo nama bora ya Ibada.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.