MTANGAZAJI

JIJI LAFUNGULIWA KESI KWA KUMFUKUZA KAZI MWADVENTISTA


Idara ya Haki ya Marekani (DOJ) imefungua kesi ya ubaguzi wa kidini dhidi ya jiji la Lansing, Michigan, Marekani, kwa madai ya kumfukuza kazi muumini wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato la Lansing, Sylvia Coleman kwa sababu alikataa kufanya kazi siku ya Sabato, ikiwa ni ukiukaji wa sheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Marekani ya Haki za Kiraia ya 1964 .

Katika malalamiko  yaliyowasilishwa Julai 15, 2022, Sylvia anasema aliajiriwa kuwa afisa anayehusika na masuala ya kizuizini mwaka wa 2018 baada ya kuwaarifu maafisa wa idara ya polisi na idara ya rasilimali watu kwamba hatopatikana  kufanya kazi kuanzia Ijumaa machweo hadi machweo Jumamosi, badala ya kuchukua hatua za kumpangia ratiba nyingine jiji lilimfukuza Sylvia mara moja.

DOJ inatafuta malipo ya kurudi kazini pamoja na riba,ikiwemo  fidia  kwa Sylvia. Zaidi ya hayo, inataka jaji atoe amri ya kuzuia jiji kuwabagua wafanyakazi kwa misingi ya dini na kuamuru jiji kuunda na kutekeleza sera ambazo zinaweza kuzuia ubaguzi wa kidini.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Mwanasheria wa Jiji la Lansing Jim Smiertka anakanusha madai hayo, akisema, Hawaamini kwamba yaliyosemwa yanapatana na yanaendana  na ukweli na sheria kama wananavyoijua.

Kwa mujibu wa taarifa ya DOJ kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa "Ubaguzi wa kidini na kutovumiliana hauruhusiwi mahali pa kazi leo," Mwanasheria Mkuu Msaidizi Kristen Clarke wa Kitengo cha Haki za Kiraia cha Idara ya Haki amesema katika taarifa. "Wafanyakazi hawapaswi kuchagua kati ya dini yao na riziki yao, haswa wakati mwajiri anaweza kukubaliana na imani zao za kidini."

Kwa mujibu wa malalamiko hayo, Sylvia alifanya usaili wa nafasi ya kazi  Desemba 2017, na wakati wa mahojiano yake aliwafahamisha kuwa hangeweza kufanya kazi kuanzia Ijumaa jua linapozama hadi Jumamosi jua linapotua ili kutunza siku ya Saba ya Juma kwa kuwa yeye ni Mwadventista wa Sabato.

Juni 21, 2018, Coleman alipokea barua ya kusimamishwa kazi, ikimjulisha kwamba "kuanzia Juni 20, 2018, Jiji la Lansing litaondoa ajira yako kwa sababu huna uwezo wa kutimiza matakwa ya ajira  





No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.