MTANGAZAJI

AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA WAISLAMU

 

Polisi wamemkamata mshukiwa wa mauaji ya wanaume wanne wa Kiislamu huko Albuquerque, New Mexico,Marekani.

Wachunguzi waliifuatilia gari aina ya Volkswagen sedan yenye vioo vyeusi inayodaiwa  kuendeshwa na mshukiwa wa mauaji ya hivi karibuni, Mkuu wa Polisi wa Albuquerque Harold Medina alitangaza wakati wa mkutano wa wanahabari Jumanne mchana.

Gari hilo lilisimamishwa na Polisi wa Jimbo la New Mexico karibu na Santa Rosa, New Mexico -- kama maili 115 mashariki mwa Albuquerque -- baada ya taarifa  kutoka kwa mwananchi  kufuatia kutolewa kwa maelezo ya gari hilo.

Dereva wa gari hilo, alimetambuliwa kuwa ni Muhammad Syed mwenye umri wa miaka 51.

Wanaume wanne Waislamu wameuawa katika kipindi cha miezi tisa katika kile ambacho polisi wamekitaja kuwa huenda ni mwendelezo wa mauaji.

Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa Mauaji ya hivi punde zaidi yalitokea siku ya Ijumaa, wakati Naeem Hussain, mzaliwa wa Pakistani mwenye umri wa miaka 25, alipokutwa  amefariki kutokana na jeraha la risasi karibu na Mtaa wa Truman na Grand Avenue huko Albuquerque .

Muhammad Afzaal Hussain, 27, alipatikana akiwa ameuawa kwa kupigwa risasi Agosti 1, na Aftab Hussein, 41, mnamo Julai 26, polisi wamesema. Wanaume wote wawili wanatoka Pakistan.

Mohammad Ahmadi, Muislamu kutoka Afghanistan, aliuawa Novemba mwaka jana nje ya biashara aliyokuwa akiendesha na kaka yake, polisi wamesema.

Baada ya Syed kukamatwa, polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake, ambapo silaha kadhaa zilipatikana, bunduki moja ilipatikana ndani ya nyumba na nyingine ilipatikana ndani ya gari ambayo inahusishwa na matukio ya mauaji hayo.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.