MTANGAZAJI

MAHAKAMA YAONGEZA KIFUNGO KWA WALIOFUNGWA MAISHA

 
Wanaume watatu wanaotumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya Ahmaud Arbery wamehukumiwa tena Jumatatu  na mahakama ya Kaunti ya Glynn,Brunswick,Georgia  kifungo cha muda mrefu gerezani kwa mashtaka ya uhalifu wa chuki.
Travis McMichael, ambaye alimpiga risasi Arbery, atatumikia kifungo chake cha maisha pamoja na miaka 10. Huku Baba yake, Gregory, ambaye alianzisha harakati za mauaji, atatumikia jela ya maisha pamoja na miaka saba.
Jirani yao William "Roddie" Bryan, ambaye alichukua video ya mauaji hayo, alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela.
Watu hao Watatumikia vifungo kwa mujibu wa sheria ya nchi  kwa wakati mmoja na kifungo kwa mujibu wa sheria za majimbo. Hakimu alikataa ombi la kila mmoja wao  Jumatatu kutumikia vifungo vyake katika jela ya umma.
Mnamo Februari, Mahakama iligundua kuwa wanaume hao watatu, ambao ni wazungu, walikiuka haki za kiraia za Arbery na walimlenga shabaha kwa sababu ya rangi yake. Arbery alikuwa Mweusi
Arbery(25) aliuawa Februari 23, 2020, baada ya akina McMichael kunyakua bunduki na kuruka kwenye gari na  kumkimbiza baada ya kupita pembeni mwa nyumba yao huko Brunswick.
Bryan, 52, alijiunga na kumfukuza kwa kutumia gari yake lake, alisaidia kuzuia kukimbia kwa Arbery na kurekodi video kwa kutumia simu tukio la mauaji hayo.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.