ALIYEWAHI KUWA KIONGOZI WA WA ADVENTISTA AFARIKI
Asubuhi ya Julai 23, 2022, Daniel R. Jackson, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato katika Divisheni ya Amerika Kaskazini (NAD) alifariki dunia baada ya miezi kadhaa ya kuugua saratani. Alikuwa na umri wa miaka 73.
Jackson, ambaye alitumikia Kanisa la Wa Adventista wa Sabato kwa miaka 49, alistaafu Julai 2020 baada ya kuhudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika Kaskazini (NAD) kwa muongo mmoja.
Akiwa mwenyekiti ,Jackson alishiriki kikamilifu katika Divisheni hiyo wakati wa huduma yake ya miaka 10 katika kitengo hicho, ikiwemo kujengwa kwa Chama cha Wachungaji wa NAD; kuundwa kwa mpango mkakati wa utume na kuongezwa kwa utume wa Guam-Micronesia, Chuo Kikuu cha Oakwood, Jumuiya ya Nyumba ya Uchapishaji ya Pacific, AdventSource, na Huduma za Utunzaji wa Kumbukumbu za Waumini wenye ulemavu wa kutoona.
Pia alihusika katika maamuzi ya Ofisi za Divisheni kuhamia kwenye makao yake makuu huko Columbia, Maryland, mnamo 2017, taarifa za matoleo zikitolewa kwa ukamilifu,kuanzishwa kwa makanisa karibu 1,000 na watu 300,000 wakibatizwa na kuimarika kwa utume wa vyombo vya habari ikiwemo vilivyoko katika eneo hilo ikiwemo Breath of Life, Faith for Today, It Is Written, Escrito Está, Jesus 101, La Voz de la Esperanza, Lifetalk Radio,Sauti ya Unabii na matumizi ya Kidigitali katika utume wa Kanisa hilo.
Jackson alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Divisheni ya Amerika Kaskazini Juni 28, 2010, na wajumbe wa kanisa hilo duniani katika Kikao cha Konferensi Kuu huko Atlanta, Georgia, na kuchaguliwa tena kwa nafasi hiyo Julai 6, 2015, katika Kikao cha 60 cha Konferensi Kuu kilichofanyika San Antonio, Texas. Kikao cha Konferensi Kuu ndicho chombo cha juu zaidi cha uongozi katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani.
Jackson mzaliwa wa Canada japo ilihudumu miaka mitano katika Divisheni ya Kusini mwa Asia, aliishi na kuhudumu katika Divisheni ya Amerika Kaskazini.Alikuwa mhitimu wa Chuo cha Unioni ya Canada (sasa Chuo Kikuu cha Burman) na Chuo Kikuu cha Andrews, ambako alihitimu Shahada ya Udhamili katika Dini na Thiolojia, Jackson alikuwa mmoja wa waandishi wa kitabu cha Becoming a Mission-Driven Church.
Post a Comment