MTANGAZAJI

MHADHIRI WA CHUO CHA WA ADVENTISTA AKABILIWA NA MASHTAKA

 


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kaskazini ya  Karibiani  (NCU) kinachomilikiwa na Kanisa la Wa Adventista wa Sabato, Russel McLean (65) ambaye alikamatwa huko Jamaica amerejeshwa Florida, Marekani hivi karibuni, kukabili mashtaka 16, yakiwemo unyanyasaji wa kingono, wizi wa nyumba na utekaji nyara.

Wachunguzi wamedai kuwa  Russell Mclean alihusika na shutuma kadhaa za ngono zilizotokea kati ya Juni 1996 na Novemba 1997 huko Margate, Florida., U.S.

Imeelezwa kuwa  McLean angeingia ndani ya nyumba na kuwatishia waathiriwa kwa bunduki ili kuwashambulia. Licha ya waathiriwa  wote kutoa maelezo sawa ya mshukiwa, uchunguzi ulikuwa na vidokezo vichache, na hakuna washukiwa waliotambuliwa,imeripoti Local10.com.

Mnamo 2007, ushahidi uliopatikana katika kesi ya wizi ulisababisha kutambuliwa kwa McLean kama mhusika. Wakati wa uchunguzi, McLean alikimbilia Jamaica, maafisa wamesema.

Hata hivyo, kwa miaka kadhaa iliyofuata, uchunguzi uliokuwa ukiendelea haukuweza kumhusisha zaidi.

Mwaka 2015, Mpelelezi Julio Fernandez alianza kuchunguza tena kesi hiyo. Mnamo mwaka  2018, Fernandez alipata ushahidi wa DNA na akalinganisha na DNA iliyo katika vifaa vya ubakaji kutoka 1996. Matokeo yalikuwa ya uhakika kwamba DNA ya McLean ilikuwa inafanana.

Mnamo Agosti 2020, hati ya kukamatwa kwa makosa mengi ya unyanyasaji kingono, utekaji nyara na wizi wa kutumia silaha ilitolewa kwa McLean.

Mnamo Mei 24, 2022, McLean alikuwa Jamaica, ambapo alikuwa akihudumu katika kitivo cha NCU, ambayo ni taasisi ya Waadventista wa Sabato.

McLean alikuwa mhadhiri katika kitivo cha Utu, Tabia na Sayansi ya Jamii, na amekuwa akifanya kazi katika NCU kwa zaidi ya miaka 18, iliripoti Jamaica Observer.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.