MTANGAZAJI

WADAU WAHOFIA ONGEZEKO LA UTOAJI MIMBA UINGEREZA NA WALES

  Idara ya Afya na Utunzaji wa Jamii imetoa takwimu za hivi karibuni za matukio ya utoaji  mimba kwa Uingereza na Wales. Kwa jumla, utoaji mimba 214,869 ulifanyika mwaka wa 2021. Hii ndiyo idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Uingereza na Wales. Pia ni ongezeko la 4,009 kutoka 2020.

Ongezeko hili kubwa limeambatana na mwaka wa kwanza kamili ambapo utoaji mimba wa wahusika wenyewe ulipatikana nchini Uingereza na Wales.

Jumla ya utoaji mimba kote Uingereza tangu Sheria ya Utoaji Mimba ilipoanzishwa mwaka wa 1967 sasa imefikia karibu milioni 10.Taasisi za Dini zinaeleza kuwa  Hiyo ni takwimu ya kushangaza na ya kuhuzunisha kwa jamii yetu kuzingatia.

James Mildred Mkurugenzi wa Mawasiliano na Ushirikiano katika shirika la CARE anasema Taasisi za dini zinahitaji  kutambua kwanza kwamba idadi ya utoaji mimba itaongezeka tu hadi sheria zibadilike, na mioyo ibadilike. Sheria  za sasa ni kuelekea kufanya utoaji wa  mimba kupatikana zaidi.

Takwimu za mwaka 2019 zinaonesha kuwa robo ya mimba kwa mwaka huo  ziliishia kwa wahusika kuzitoa

Mtandao wa Christian Today unaonesha kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (ONS) katika nchi hizo ilikusanya taarifa ya mimba 821,809 miongoni mwa wakazi nchini Uingereza na Wales kwa mwaka 2019 ambapo mimba 207,384 zilizotolewa.

 Taarifa hiyo inatanabaisha  kuwa takwimu za utoaji mimba miongoni mwa wanawake katika nchi hizo ziliongezeka kutoka asilimia 24 kwa mwaka 2018 na kufikia asilimia 25.2 kwa mwaka 2019.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.