MTANGAZAJI

IDADI YA WAMAREKANI WANAOMWAMINI MUNGU YASHUKA-UTAFITI

 


Ingawa asilimia  81 ya watu wazima nchini  Marekani wanasema wanamwamini Mungu, asilimia hiyo imeshuka kwa pointi 6 tangu 2017 na ni ya chini zaidi tangu kampuni ya Utafiti ya Gallup  ilipoanza kufanya utafiti kwa kuuliza swali hilo zaidi ya miongo saba iliyopita.
Gallup inasema ilipouliza swali hilo kwa mara ya kwanza mwaka wa 1947 na mara mbili katika miaka ya 1950 na 1960, asilimia 98 ya wamarekani walisema wanamwamini Mungu. Mnamo 2011,  ilipungua hadi asilimia  92 Katika 2013, 2014 na 2017, ilipungua hadi asilimia 87.
Matokeo ya kura ya utafiti huo yanaonesha kuwa Imani katika Mungu imeshuka zaidi katika miaka ya hivi karibuni miongoni mwa vijana,watu wazima na watu wa mrengo wa  kushoto katika siasa, Makundi haya yanaonyesha kushuka kwa asilimia 10 au zaidi ikilinganishwa na takwimu za 2022 na wastani wa 2013 na  kura za 2017.
Kura ya maoni inabainisha kuwa ni asilimia 72 tu ya Wanademokratiki, 62% ya waliberali na 68% ya vijana ndio wanaomwamini Mungu.
Kwa kuangalia imani katika Mungu kieneo, kura ya maoni iligundua kuwa Kusini ina idadi kubwa zaidi na kwa  86%, lakini ni chini kutoka 93% mwaka 2017. Kanda yenye idadi ya chini ni Mashariki ikiwa na  78%.
Kura ya maoni pia iligundua kuwa karibu robo tatu ya Wamarekani wenye dini ambao huhudhuria ibada kila juma wanaeleza kuwa wanaamini kwamba Mungu husikia maombi na anaweza kuingilia kati na ni asilimia 30 pekee ya vijana wanaoamini katika jambo hilo.
Disemba iliyopita, Gallup aligundua kuwa 49% ya Wamarekani walisema dini ni "muhimu sana" katika maisha yao, asilimia wengine 27% wakisema "ni muhimu kiasi  na 25% wakisema "sio muhimu sana”
Gallup alibainisha kuwa ilipouliza swali hili kwa mara ya kwanza mwaka wa 1965, asilimia 70 walisema dini ni muhimu sana. Hiyo ilishuka hadi 52% katika uchunguzi wa 1978 - ingawa asilimia ilipungua hadi karibu 60% kati ya 1990 na 2005, kabla ya kupungua katika miaka 15 iliyopita.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.