MTANGAZAJI

NDOA KWA WATOTO WA KIKE BADO NI TATIZO AFRIKA

 


Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na kuhudumia watoto UNICEF limezindua ripoti inayofichua kwamba wasichana wengine milioni 45 Kusini mwa Jangwa la Sahara watakuwa wamejiingiza katika ndoa za utotoni katika muongo ujao ikiwa maendeleo ya kukomesha tabia hiyo hayataharakishwa.

Marie-Pierre Poirier, Mkurugenzi wa UNICEF wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati anaangazia kwamba katika maeneo ya vijijini maskini ambayo yana kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni,ambapo ametoa wito kwa makanisa katika eneo hilo kutoa elimu ya kukomesha jambo hilo.

Amesema Juhudi zinafanywa na washirika wa kanisa katika kukabiliana na ndoa za utotoni kwa kutoa elimu kwa walezi, viongozi wa dini, mamlaka za mitaa na wazazi ili kuhamasisha uelewa wa haki za watoto wa kike, umuhimu wa elimu yao na hatari zinazoambatana na ndoa za utotoni.

Djamila ni msichana toka Burkina Faso anasema Baba yake alipanga kumwoza kwa mwanamume mzee kabla ya kutimiza miaka 15. Mbaya zaidi baba hakumshauri Djamila wala mama yake kuhusu nia yake. Licha ya umri halali wa kuolewa nchini humo kuwa ni miaka 17, UNICEF inaripoti kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wasichana huolewa kabla ya miaka 18, huku asilimia 10 wakifunga ndoa kabla ya umri wa miaka 15.
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.