MTANGAZAJI

GHARAMA ZA MAISHA UINGEREZA SABABU YA KUFIKIRIA KUJIUA

 


Watu zaidi walio na kipato cha chini nchini Uingereza wanafikiria kujiua huku gharama za maisha zikizidi kupanda, shirika la Kikristo la kutoa ushauri nasaha kwa madeni limeonya.

Shirika la Kikristo la kupambana na umasiki (CAP) limegundua  kuwa zaidi ya theluthi moja ya wateja wake ambao ni asilimia 36 walijaribu au kufikiria kujiua kabla ya kutafuta usaidizi wa madeni yao kutoka kwa mashirika ya hisani, kutoka asilimia 28 ya mwaka uliopita.

Utafiti wa CAP pia umebaini kuwa masuala ya afya ya akili yalikuwa ya kawaida, huku wateja wa CAP ambao waliripoti kuwa na msongo waliongeza  kuongezeka kwa 71%, na wale waliosema kuwa wamepata wasiwasi waliongezeka kwa 80%.

Mteja mmoja wa CAP, Syd, alifikiria kujiua wakati ugonjwa mbaya ulimwacha na deni lisiloweza kulipwa.

Ripoti ya hivi karibuni ya mteja inaonyesha pengo kubwa kati ya deni la binafsi na kile ambacho watu wanapata. Ingawa mapato ya wastani ya wateja wa CAP ni paundi 13,404 baada ya gharama za makazi, wastani wa kilele cha deni ni paundi 17,306 - tofauti ya 3,902.

Ripoti hiyo imegundua kuwa watu nchini Uingereza wanazidi kuingia katika madeni makubwa ili tu kulipia gharama za kimsingi za maisha kama vile kodi ya nyumba, bili za matumizi na kodi ya serikali, na kupanda kwa 14% kutoka paundi 5,852 hadi paundi 6,698 katika miezi 12 iliyopita.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.